Home » » WATER REED TANZANIA WRP WATOA MSAADA WA GARI NA PIKIPIKI WENYE THAMANI YA ZAIDI YA MILIONI 267 KWA HALMASHAURI ZA MKOA WA KATAVI .

WATER REED TANZANIA WRP WATOA MSAADA WA GARI NA PIKIPIKI WENYE THAMANI YA ZAIDI YA MILIONI 267 KWA HALMASHAURI ZA MKOA WA KATAVI .

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 

  Na  Walter  Mguluchuma .
       Katavi .
 Shirika la  Water  reed  Program  Tanzani  WRP  T   limetowa msaada wa   gari moja kwa  Manispaa ya  Mpanda na pikipiki 26 kwa   Halmashauri za  Mkoa wa  Katavi    wenye  thamani ya  zaidi ya shilingi milioni 267  kwa ajiri ya  shughuli za  mradi wa  kutdhibiti  Ukimwi  Mkoani  Katavi .
Msaada huo ulikabidhiwa  hapo jana  na   Mkuu wa  Mkoa wa  Katavi  Meja  Gegerali  Mstaafu  Raphael  Muhuga kwa  Halmashauuri    zote  tano za   Mkoa wa  Katavi  katika   hafla  iliyofanyika  katika   viwanja vya   ofisi ya  Mkuu wa  Mkoa wa Katavi .
Akiwa taarifa ya  msaada huo       Reginol  Program  Maneger   WRP   T  wa  Mkoa wa  Katavi  Dr   Baraka   Mgiriwa alisema  msaada huo wa  gari  moja  na pikipiki  26 umegharimu  kiasi cha   Tshs 267,789.707 milioni.
Alifafanua kuwa  katika  msaada huo  Manispaa ya  Mpanda wamepata   gari moja   aina ya  Picup  Land  Cruzan a   lenye  thamani ya  Tshs  168,987.707  Milioni   pikipiki  4  aina ya  Honda , Halmashauri ya  Mpanda pikipiki  5,   Mlele  pikipiki  5, Nsimbo pikipiki   6, Mpimbwe pikipiki  5 na   ofisi ya  Mganga   Mkuu wa   Mkoa   pikipiki  moja   zikiwa  na  thamani ya   Tshs  98,800,000.
Mganga   Mkuu  wa  Mkoa wa  Katavi  Dr   Yahaya  Huseein alieleza kuwa    baada ya  Halmashauri  kukabidhiwa msaada huo  wanamatarajio  makubwa ya  kutowa  huduma   mbalimbali  katika  maeneo ya  Halmashauri hizo   alizitaja baadhi ya huduma  hizo kuwa ni .
 Kuimarika  kwa  shughuli  za usarishaji wa  sampuli  kavu  za damu  za watoto  waliozaliwa  na mama   wenye  maambukizi ya VVU  kwa  ajiri  ya kupimwa  hali ya maambukizi .
Kupunguza  uharibifu  wa  sampuli  za  damu  kwa watoto  waliozaliwa  na mama  wenye VVU   pamoja  na zile  za  kupima  wingi  wa kiwango  cha vvu  katika  damu  kwa  WAVIU  wote  kwa kuchelewa  kusafirishwa   kwenda katika  maabara.
 Dr  Yahaya   alitaja  matarajio  megine  kuwa ni  kuongeza  uchukuaji  na usafirishaji  wa  sampuli  za  damu  kwa  ajiri ya  kupima  wingi wa  VVU  katika  damu  kwa  WAVIU  ili kuweka tiba   sahihi  kwa wale  watakao kuwa  na idadi  kubwa  ya  kiwango  cha vvu  katika  damu .
Pia  wanatarajia  kutekeleza  shughuli   zote  zilizo hainishwa  katika mpango kwa  wakati na kwa haraka  kwa kutumia   vitendea  kazi  hivyo  walivyo  kabidhiwa  na  WRP..T.
Mkuu wa  Mkoa wa  Katavi Raphael  Muhuga  alisema kuwa  msaada huo utasaidia sana  kuboresha  utendaji kazi  kwa wagonjwa  kupatiwa huduma kwa wakati tofauti  na ilivyokuwa  hapo   awali .
Na alizisisitiza  Halmashauri  zote za  Mkoa huo  zione   umuhimu wa   kuvitunza  vitendea kazi   hivyo na wavitumie kwa makusudi yaliokusudiwa .
Nae   Mkurugenzi wa  Halmashauri ya    Mpimbwe     Erasto  Kiwale   alisema  kuwa   kutoka na    jografia ya  Halmashauri  yake  pikikpiki   hizo   zitasaidia  watumishi wa   afya kwenda kutowa huduma kwenye maeneo   ambayo  hayafikiki kwa  gari kwa urahisi .
Diwani wa  Kata ya  Mkanyagio  Haidari Sumry  alisema   kuwa  mapambano ya  Ukimwi sio jambo dogo  hivyo  vitendea kazi hivyo  hivyo vitasaidia  wgonjwa kupa huduma kwa wingi kwa muda mfupi .


0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Katavi yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa