Na Walter Mguluchuma .
Katavi .
Mkoa wa Katavi hadi sasa unajumla ya wateja wapya na wanaondelea kutumia dawa za ARVs 13,671 ambapo ni sawa na asilimia 56 ya watu wote wanao kisiwa kuwa kuwa na maambukizi ya VVU katika Mkoa wa Katavi huku Mkoa ukiwa umefanikiwa kuongez vituo vya tiba na matunzo kutoka 11 hadi 20.
Hayo yalisemwa hapo jana na Mganga Mkuu wa Mkoa wa Katavi Dr Yahaya Hussein wakati alipokuwa akosoma taarifa fupi ya mradi wa kuthibiti Ukimwi Mkoa wa Katavi wakati wa hafla fupi ya kukabidhi gari moja la Manispaa ya Mpanda na pikipiki 26 kwa Halmashauri zote tano za Mkoa wa Katavi ikiwa ni msaada wa kutoka water red Program Tanzania WRP T hafla iliyofanyika katika viwanja vya ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Katavi .
Alisema kuanzia mwezi Januari 2017 kiasi cha wateja waliotambulika kuwa na maambukizi ya VVU na kufanikiwa kuandikishwa katika vituo tiba na mafunzo , jumla ya wateja 4,212 walifanikiwa kuunganishwa katika vituo vya huduma na matunzo hadi kufikia 30 Septemba 2017.
Dr Yahaya alifafanua kuwa Mkoa wa Katavi unajumla ya wateja wapya na wanaoendelea kutumia dawa ya ARVs 13,671 sawa na asilimia 56 ya watu wote wanaokisiwa kuwa na maambukizi ya VVU .
Mkoa utaendelea kutekeleza sera ya Wizara ya Afya kwa kuhakikisha asilimia 100 ya wajawazito wote wanahudhuria kiliniki ya akina mama wajawazito pamoja na wanaonyonyesha wote wanapimwa hari ya maambukizi na wale wanaotambulika kuwa na maambukizi ya VVU wanaunganishwa katika matibabu ya ARVs mara moja ili kumkinga mtoto aliyezaliwa na anaenyonya .
Alisema pamoja na jitihada kubwa zinazofanywa na watumishi pamoja na timu za usimamizi wa huduma ya afya ngazi ya Mkoa na Halmashauri , Mkoa bado unakabiliwa na changamoto mbalimbali katika kuendelea kutimiza malengo waliyoyaweka na alizitaja baadhi ya changamoto hizo kuwa ni .
Uhaba wa watumishi katika vituo vya kutolea huduma za CTC ambavyo vimeongezeka kutoka kumi na moja na kufikia idadi ya vituo ishirini vya huduma tiba na mafunzo kwa Mkoa mzima wa Katavi .
Idadi kubwa ya wateja wanaopotea katika dawa kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo umbali wa kufikia kwenye vituo vya tiba na mafunzo ,shughuli za kilimo na mifugo zinachangia wateja kuhama bila kutowa taarifa na kuonekana kama wateja watoro .
Alitaja changamoto yingine kuwa ni shughuli za udhibiti UKIMWI hazipewi kipaumbele cha kutosha katika kutenga rasilimali za Halmashauri husani magari na hivyo kukwamisha shughuli za mradi kufanyika kwa wakati .
Mkuu wa Mkoa wa Katavi Meja Generali Mstaafu Raphael Muhuga alisema Mkoa huo unakabiliwa na tatizo la maambukizi ya VVU hivyo jitihada kubwa zinahitajika ili kuweza kudhibiti maambukizi ya VVU .
Alisema msaada wa vitendea kazi uliotolewa na WRP T usaidia kuboresha kazi kwenye Halmashauri za Mkoa wa Katavi katika swala zima la kuthibiti Ukimwi .
Mkurugenzi wa Manispaa ya Mpanda Michael Nzyungu alisema gari moja walilopatiwa na pikipiki nne kwenye Manispaa hiyo zitasadia kupata taarifa na mapema za maambukizi ya VVU kutoka kwenye vituo vya kutolea huduma kwani hawakuwa na gari lata moja lililokuwepo kw ajiri ya huduma hiyo .
0 comments:
Post a Comment