AMATI ZA USHAURI WA KISHERIA ZAZINDULIWA KATAVI, WANANCHI WAPATIWA HUDUMA ZA SHERIA BILA MALIPO

Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali kwa kushirikiana na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Katavi, imezindua Kamati ya Ushauri wa Kisheria ngazi ya Mkoa na Wilaya katika Mkoa wa Katavi. 

Uzinduzi huo umefanyika tarehe 8 Septemba, 2026 na kufuatiwa na kliniki ya Sheria bila malipo iliyoanza tarehe 7 Septemba, 2026 katika Viwanja vya Azimio Mpanda Uzinduzi wa Kamati za Ushauri wa Kisheria na Kliniki ya Kisheria bila malipo, ni dhamira ya dhati ya Serikali kupitia Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali ya kutatua migogoro, kutoa ushauri wa Kisheria kwa wananchi na elimu ya Kisheria bila malipo. 

 Akizungumza katika hotuba yake ya Uzinduzi, Mkuu wa Wilaya ya Mpanda Mhe. Jamila Yusuph, ameeleza kuwa jukumu la kutatua migogoro katika maisha ya watanzania sio la Serikali pekee ni jukumu la wadau wote wa maendeleo. 

 Mhe. Mkuu wa Wilaya amekuwa mgeni rasmi akimwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Katavi Mhe. Mwanamvua Hoza Mrindoko katika Uzinduzi wa Kamati za Kudumu za Ushauri wa Kisheria ngazi ya Mkoa na Wilaya zimezinduliwa mkoani Katavi, tarehe 8 Septemba , 2026, katika Viwanja vya Azimio, Mpanda.

MIZENGO PINDA ATAKA WANA CCM KUJIEPUSHA NA MANENO YA UCHOCHEZI

Na Munir Shemweta, MLELE  

Waziri Mkuu Mstaafu ambaye ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama cha Mapinduzi Taifa Mhe. Mizengo Pinda amewataka wanachama CCM wanaotaka kugombea nafasi yoyote kujiepusha na maneno ya uchochezi yanayoweza kuharibu mahusiano baina yao.

 

Pinda amesema hayo tarehe 20 Julai 2024 wakati akizungumza na viongozi mbalimbali wa CCM wakiwemo madiwani, viongozi wa kata pamoja na wazee katika halmashauri ya Mpimbwe wilaya ya Mlele mkoa wa Katavi.

 

Amesema, kwa yoyote anayetaka kugombea nafasi ya uongozi ni vizuri akawa muangalifu na maneno ya uchochezi aliyoyaeleza kuwa, wakati mwingine yanaweza kumletea tabu wakati haipo.

 

"Chonde chonde sana usije ukaingia kwenye ugonjwa, unakaa unakuzungusha kicwa kwa sababu kuna mtu kaja kukuambia eeh kuma mtu fulani anakusema vibaya sasa hujathibitisha unaanza kutembea nayo na wewe usiende hivyo kwenye siasa hatuendi hivyo" amesema Mizengo Pinda

 

Amewataka wanapopelekewa maneno kuyapokea na kutulia huku wakijaribu kuyachunguza ili kuona ukweli au uongo kwa kile wanachoambiwa na kuweka wazi kuwa, wengi huponzwa na maneno ambapo amesisitiza, wana CCM kujaribu kupunguza maneno ya uchochezi yatakayosababisha kukwaruzana pasipo sababu ya msingi.

 

Kwa upande wake mbunge wa jimbo la Kavuu ambaye ni Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Geophrey Pinda ameeleza kuwa, hali ya kiasiasa ndani ya jimbo lake iko shwari na amekuwa akifanya vikao vya mara kwa mara kwa wananchi wa rika zote kupitia kata za jimbo hilo.

 

Hata hivyo, Mbunge huyo ameweka wazi kuwa, wakati mwingine kwa namna moja ama nyingine amashindwa kumfikia kila mwananchi kwenye jimbo hilo kutokana na idadi kubwa ya wakazi wake aliyoieleza kwamba imekuwa ikiongezeka siku hadi siku.

 

Amebainisha kuwa, kupitia wizara yake ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi wako mbioni  kuweka mipango ya  matumizi bora ya ardhi kwa kila kijiji ila  wanachi wapate hati milki za ardhi na kuweza kuzitumia kwa matumizi mbalimbali ikiwemo kuchukulia mikopo benki.

 


 

 

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Katavi yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa