Home » » CHAMA CHA WALIMU CWT WILAYA YA MPANDA YAOMBA SERIKALI IPOKEE CHANGAMOTO ZAO NA KUWAPA MAJIBU YA UATATUZI WA KERO ZAO .

CHAMA CHA WALIMU CWT WILAYA YA MPANDA YAOMBA SERIKALI IPOKEE CHANGAMOTO ZAO NA KUWAPA MAJIBU YA UATATUZI WA KERO ZAO .

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 
 


  Na  Walter  Mguluchuma .
  Katavi .
  Chama cha  Walimu   Tanzania   CWT  wilaya  ya Mpanda  Mkoani  Katavi  kimeiomba  Serikali  ipokee   changamoto  zinazowabili Walimu  ambao ni   wanachama  wao  na kuwapatia  majibu  yatakayo uonyesha  utatuzi wa  kero  zinazowakabili Walimu .
Ombi hilo  lilitolewa  hapo jana  kwenye risala  yao  kwa   Mkuu wa  Mkoa wa  Katavi  wakati wa Mkutano Mkuu wa  Chama  cha  Walimu  Wilaya ya  Mpanda uliofanyika  katika  ukumbi wa  Mtakatifu  Maria    ilisomwa  na  Katibu wa   CWT   Wilaya  ya   Mpanda   Wilson  Masolwa.
 Masolwa   alisema   Chama    cha Walimu  Tanzania CWT  Wilaya ya Mpanda  kinaiomba  Serikali  ipokee  changamoto  zinazowakabili  Walimu  ambao ni wanachama  wa  chama  hicho  na kuwapatia majibu  yakakayo onyesha  utatuzi wa kero zao .
Alieleza kuwa  Chama cha Walimu  kinataka kujua  ni kwnini  PSPF   wanaendelea  kukata  fedha  za kunua mgongo  kwa walimu  wastaafu  ambao haikuwa jukumu lao  kuwasilisha  makato  kwenye mfuko wa  PSPF .
 Kero  nyingine waliitaja kuwa ni  wastaafu  kuendelea  kucheleweshewa  malipo yao  ya kinua mgongo  chao kipindi  ambacho wanapokuwa wamestaafu na kuwaletea usumbufu  walimu wo wastaafu .
 Alisema  Chama cha  Walimu  kinaiomba   Serikali  kuwasimamia  waajiri wa mifuko  ya Hifadhi ya Jamii kutowachelewesha  walimu wastaafu  kuwarudisha kwao  mara tuu wanapo   hitimu  utumishi wao wa umma .   kuanzia  tarehe ya kustaafu  na  kama   mifuko  inapochelewesha  malipo  zaidi ya siku  60 na sababu za kuchelewesha  malipo  hazitokani   na  mstaafu  mfuko ukubali  kulipa tozo  la asilimia 15 ya kiwango  anachostahili kwa  mwaka .
Mwenyekiti wa  CWT  Wilaya ya  Mpanda  Jumanne   Msomba   alieleza kuwa  Chama  hicho  kimefanya  mambo mengi hadi sasa kwa  wanachama wake  na  kwa maendeleo ya ya  sekta ya  elimu .
  Alitaja baadhi ya  mambo ya maendeleo yaliofanya na chama hicho kuwa   wameweza  kuchangia   mchango  wa  madawati  20 kwa  shule ya msingi   Mnyagala  yenye  thamani ya Tshs 2,500,000 saruji  kwenye  shule  ya  Msingi  Kasekese na  Sekondari ya  Mpanda  Ndogo yenye thamani ya  Tshs  9,000,000.
Pia  wamekuwa wakiwapatia   bati  20 kwa  kila  mwalimu  ambae     anakuwa   amestaafu na  zoezi   hilo huwa  linafanyika  kila mwaka  bila   kujari idadi ya walimu  wanaokuwa  wamestaafu   kwa  mwaka huo.
Na  wamekuwa  wakitowa  motisha   kwa  Shule  zilizofaulisha    vizuri  matokeo ya  kidato cha  sita na  na  darasa la saba  pia  wameweza  kuwawezesha  walimu  46 kupata viwanja  vya makazi   eneo la  Mapinduzi Manispaa ya  Mpanda .
Mwenyekiti wa   CWT  Mkoa wa  Katavi  John  Mshoto  aliwataka  Walimu  ambao ni  wanachama wa  Chama  hicho kuacha kubaguana   kati ya  walimu wa Shule za  Msingi na  Sekondari .
 Alisema kumekuwa  na  tabia ya  walimu wa  Sekondari na  washule za   Msingi  kubaguana  hata  kwenye  msiba kwa  walimu hao  pindi   misiba  inapokuwa imetokea  jambo  ambalo sio  zuri    zuri kabisa  na halikubaliwi  katika jamii.
Mwakilishi wa   Mkuu wa  Mkoa   kwenye  Mkutano huo  ambae ni  Mkuu  wa   Wilaya  Tanganyika   Salehe    Mhando   alisema  kuwa  Serikali  inajitahidi  kuhakikisha  mazingira ya walimu  yanakuwa     mazuri .
 Alisema  matatizo waliyonayo  walimu  yatatatuliwa na  Serikali kwa  hatua kwa  hatua  na  aliwaomba  Walimu  wamuunge   mkono  Rais  John  Magufuli   katika  jitihada zake za kusimamia  raslimali za   nchi  kwani  wanao  nufaika  na  jitihada za  Rais ni  Wanzania  wote.
Mkutano huu pia ulimchagua  Lucas Izack kuwa  mwakilishi wa  walimu  wenye ulemavu baada ya  kupata kura  57 na kumshinda mgombea mwenzake kwenye nafasi hiyo    Didas Kalonje alipata kura 44
MWISHO

 

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Katavi yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa