Home » » KAMPUNI YA GBP YATOWA MSAADA WA KISIMA CHA MAJI CHENYE THAMANI YA MILIONI 55.

KAMPUNI YA GBP YATOWA MSAADA WA KISIMA CHA MAJI CHENYE THAMANI YA MILIONI 55.

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 


  Walter  Mguluchuma   Na  Arine  Temu 
       Katavi .
Mampuni ya  mafuta ya  GBP  imekabidhi  kisima  cha   maji      chenye   thamani ya    shilingi  milioni 55  ikiwa  ni  msaada  kwa   ajiri ya  Wakazi wa  Kata ya  Majengo  Manispaa ya   Mpanda  chenye  uwezo wa  kutowa  maji zaidi ya  lita  za  ujazo     1,400  kwa  siku .
Meneja wa  Kampuni ya GBP   alikabidhi kisima  hicho  hapo  jana  kwa  niaba ya   kampuni   hiyo  kwa   Diwani wa  Kata ya  Majengo Willy  Mbogo   katika   hafla  iliyofanyika     katika   eneo la  kisima  hicho  katika   Mtaa wa  Majengo 
Katika  hotuba  yake  wakati   akikabidhi  kisima  hicho   Meneja wa  GBP  Mpanda   Hamad   Nassor  Said   alisema  kuwa kisima  kicho   kimegharimu  kiasi  cha  shilingi  milioni 55  na  kinazalisha   maji  lita  za  ujazo  1460 kwa  siku .
Alisema  lengo la  kampuni  kutowa msaada  huo kwa  wananchi  wa  Kata  hiyo ni   katika  kuwapunguzia  wananchi   tatizo  la  upungufu wa  maji  kwenye  eneo la   Kata  hiyo   ambayo ipo  kati  kati ya   Mji wa  Mpanda .
Meya  wa  Manispaa ya  Mpanda   Willy  Mbogo   ambae ni  Diwani wa  Kata ya  Majengo   aliishukuru  kampuni  hiyo  kwa  kutowa   msaada  huo  muhimu wa  kisima    cha  maji   ambacho  alisema  kitakuwa ni msaada  mkubwa  si  kwa wakazi wa  Kata ya  majengo peke   yake  bali na   Kata  zilizo   jirani .
 Alisema  msaada  huo  ni  muhimu kwani   hakuna   mtu yoyote  duniani  ambae kila  siku  hatumii  maji kwa   ajiri ya  kunywa ,kuoga ,kufua na  kupikia    pamoja na  kuoshea  vyombo .
Mbogo  aliwataka  wananchi  kuhakikisha  wanatunza   vizuri  miundo  mbinu  hiyo  kwani  kumekuwa na tabia  ya  baadhi ya  wananchi  kutuma  watoto  kwenda  kuchota  maji na  matokeo yake  wamekuwa wakiharibu   miundo  mbinu  hivyo  wajenge  tabia ya kuwatuma  watoto wao  wenye  uwelewa  na sio watoto wadogo zaidi .
Mwenyekiti wa  Mtaa  huo wa  Majengo   Maga   Athanas   alisema  kuwa   kisima  hicho  kitakuwa  ni   mkombozi kwa   akina  mama  kwani  walikuwa  wakipata   shida   kubwa ya   maji  kutokana  na     eneo  hilo la  majengo  kutokuwa  na  maji ya  uhakika .
Nae  Mashaka   Rubuye  alisema  kuwa  watu  wengi   watafaidika  na   maji ya  kisima   hicho  kwani  watu watakuwa  wanachota  bure   tofauti  na  kwenye  maeneo  mengine  ambapo   maji  huwa  wanauziwa    ndoo  moja  kati ya  Tshs 200.
mwisho
  
    

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Katavi yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa