Home » » MEYA WAMANISPAA YA MPANDA KAKUSHA KUHUSISHWA NA KUGOMBEA UBUNGE.

MEYA WAMANISPAA YA MPANDA KAKUSHA KUHUSISHWA NA KUGOMBEA UBUNGE.

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 


Na  Walter  Mguluchuma
      Katavi .
Meya wa  Manispa ya  Mpanda  Willy  Mbogo  amekanusha  vikali taarifa  ambazo  ambazo vimeenea katika  maeneo mbali mbali ya  Mkoa wa  Katavi za kuwa  yeye  anao mpango wa kugombea ubunge kwenye uchaguzi mkuu  ujao wakati  jambo hilo   halina  ukweli wowote   kwani yeye  hana  mpango wa kugombea  ubunge  kwenye  jimbo lolote la  Mkoa wa  Katavi
Mbogo  ambae  ni   Diwani wa  Kata ya   Kashauli    CCM  alitowa  kauli  hiyo jana   wakati alipokuwa  akiwahutubia   wananchi wa   Kata ya  Majengo wakati wa uzinduzi wa  kisima cha   maji  kilichojengwa na   Kampuni ya kuuza  mafuta ya GBP  kilichogharimu kiasi cha  shilingi  Milioni 55 ikiwa ni  msaada  uliotolewa  na  Kampuni  hiyo .
Alisema  yeye  amekuwa  akizushiwa  kuwa  anao  mpango wa kugombea  ubunge  katika  Jimbo la  Mpanda   Mjini  jimbo  ambalo   linaongozwa  kwa  sasa   na  Sebastiani  Kapufi .
 Alisema  kuwa    napenda  kuwahakikishia  wakazi wa    Manispaa ya  Mpanda  na  wananchi wa  Mkoa wa  Katavi kwa ujumla wake kuwa  yeye  hana  mpango wa kugombea  ubunge kwenye uchaguzi mkuu ujao wa  2020  kwenye  jimbo  lolote la  Mkoa wa  Katavi.
 Alifafanua  kuwa  nafasi ya udiwani  aliyonayo  inamtosha  sana   hivyo   ataendelea kuwatumikia   wananchi kwa  nafasi  hiyo ya  udiwani  kwani inamfanya kila  siku   kufanya kazi ya kuwatumika wananchi kwa  karibu  zaidi.
Nimekuwa  nikuzushiwa  mara  kwa  mara  kuwa  anampango wa kugombea  udiwani  na  hata  hivi  karibuni  wakati wa   mkutano   mkuu wa  CCM  wa  Wilaya ya  Mpanda   baadhi ya  wajumbe wa mkutano huo walihoji  swala  hilo  alisema  Mbogo .
Alisema  ameamua  kukanusha  swala  hilo  mapema  kwani   anaona  siku  hadi  siku  watu  wanaendelea kuzusha  swala hilo  ambalo yeye  wala  haliko   hata  moyoni  mwake kwa  sasa wala  wala  hakilii  kabisa zaidi ya  kuwaendelea kuwatumukia  wananchi wake kwa  nafasi ya udiwani.
 Alieleza kuwa  wakati wa  mkutano Mkuu wa  uchaguzi uliofanyika   yeye   aligombea  ujumbe wa  mkutano  mkuu wa  Taifa  na    aliweza  kushinda   nafasi  hiyo  licha ya  watu  ambao  walikuwa  wameanza kumzushia  kuwa  kwanini   agombee  nafasi hiyo wakati pia  anampango wa kugombea  ubunge kwenye  uchaguzi  mkuu   ujao .
MWISHO

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Katavi yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa