Home » » TANESCO KATAVI KUANZA KUTOWA ELIMU KWENYE MASHULE

TANESCO KATAVI KUANZA KUTOWA ELIMU KWENYE MASHULE

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 


  Na  Walter  Mguluchuma
          Katavi
 Shirika  la umeme  Tanzania  TANESCO   Mkoa  wa  Katavi  limepanga kuanza kutowa elimu  kwenye  shule za Msingi na  Sekondari zilizopo   katika  Mkoa huu  ili kuwafanya Wanafunzi wafahamu zaidi madhara yanatokana  na Umeme .
Hayo yalisemwa  hapo jana   na  Afisa   mawasiliano  na  wateja wa TANESCO  wa  Mkoa wa  Katavi   Amoni    Maiko wakati alpokuwa akizungumza na   baadhi  ya  wateja wa shirika  hilo  katika  Kijiji  cha  Songambele   Tarafa ya  Nsimbo    Wilaya ya Mlele waliokuwa wakililalamikia  shirika hilo  liwalipe fidia kutokana na hasara walioipata ya kuunguliwa na baadhi ya vifaa kutokana na  tatizo la kukatika kwa umeme uliotokea mei 28 mwaka huu.
 Alisema  watu  wengi wameuzowea  sana umeme ni kama vile  huwa hausababishi kifo na kujisafirishia umeme  bila kupitia  wataalamu  wa Tanesco  wakati jukumu la kusafirisha na kusambaza umeme ni la Tanesco  hivyo  TANESCO  Katavi kwa kulitambua hilo imepanga kuanza kutowa elimu kuanzia  kwa Wanafunzi  wanaosoma  kwenye  shule za Msingi  na  Sekondari ili waweze kufahamu  madhara ya umeme wakati wangali bado wako wadogo .
  Afisa  huyo  Mahusiano   aliwaeleza  wananchi  hao   kuwa  watu waache  tabia  ya kupeana umeme  bila kufuata  taratibu  kwani kufanya  hivyo ni kosa na  adhabu yake ni shilingi  laki   tano  na  pia  wawatumia wakandarasi  wanaotambulika na shirika  bindi wanapokuwa wanafanya  matengenezo ya umeme kwenye  nyumba zao .
Akijibu swali lililoulizwa  kuhusiana  na  kukatika kwa umeme  katika  maeneo  mbalimbali lililoulizwa na   Lucas  Maganga  mkazi wa   Kijiji   hicho   Afisa  Mahusiano  Amoni   Maiko  alisema  kukatika kwa umeme kumekuwa kukisababishwa  na  sababu  nyingine  ambazo  zipo   nje ya  shrike  la  Tanesco .
  Alizitaja  baadhi ya      sababu  zinazosababisha kukatika kwa umeme  kuwa ni   gari kugonga nguzo ya umeme ,  mti kuangukia kwenye waya wa umeme  na  wezi  wanaoiba  mafuta  kwenye   Transifoma.
 Sasa  hivi shirika   lipo linaendelea  kuwakamata  watu wanaoiba  umeme   na limekuwa likiwapatia   zawadi watu  ambao  wanaotowa  taatifa ya kukamatwa kwa wezi  na  zawdi  hizo wamekuwa wakizitowa kwa usiri hivyo ni vema watu wakaendelea kutowa ushirikiano kwa Tanesco ili kusaidia kuwabaini watu wanaoiba umeme
Nae  Deo  Mwaisaka  Mkazi wa  Kijiji  hicho  cha  Songambelea  ambao  wamepata  umeme   hivi  karibuni  kupitia  mpango wa Rea   Yassin  Nasibu  aliliomba  shirika  la  Tanesco  kuwa na utaratibu wa kuwapatia  elimu ya mara kwa mara wateja wake  iliwaweze kuepukana  na  madhara kabla  hayajatokea
 .
 Alisema  watu  baadhi   hawana  elimu   na  ndio  maana  hata  wanapokuwa wamekuwa wakipata  tatizo  huwa   hawajuwi watowe  taarifa  wapi .
Faustina  Method alieleza  kutoka na kutokuwa  elimu ya kutosha  kwa  baadhi  ya  wateja wa Tanesco  hasa waliopatiwa  umeme wa  Rea wamekuwa  hawatowi taarifa kwa shirika pindi  wanapotaka  kuongeza   ramani ya miundo mbinu yao hari ambayo imekuwa ikiwasababishia washindwe kudai  haki zao  pindi yatokeapo  madhara ya umeme kwenye  nyumba zao .

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Katavi yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa