Na Walter Mguluchuma
Katavi
Kikao cha Halmashauri kuu ya CCM Wilaya Ya Mpanda Mkoa wa Katavi imetowa matamko manne yakiwamemo ya kuziagiza Halmashauri za Wilaya ya Mpanda na Manispaa ya Mpanda kukamilisha ujenzi wa Zahanati ifikapo Agosti 30 ilzianze kutowa huduma kwa wananchi na kukifunga kiwanda cha kusindika mafuta kinachomilikiwa na Halmashauri ya Wilaya ya Mpanda.
Kikao hicho cha Halmashauri kuu ya CCM Wilaya ya Mpanda kilifanyika hapo juzi katika ukumbi wa Ccm Wilaya ya Mpanda kiliongozwa na Mwenyekiti wa chama hicho wa Wliya hiyo Beda Katani .
Mwenyekiti wa CCM wIlaya ya Mpanda Beda Katani aliwaambia Waandishi wa Habari jana kuwa kikao hicho kilitowa matamko manne ya kuziagiza Halmashauri za Wilaya ya Mpanda na Manispaa kutekeleza maazimia ya kikao hicho .
Katani aliyataja maazimio hayaliyotolewa na kikao hicho kwa Halmashauri ya Wilaya ya Mpanda ni kuwa ihakikishe iwe imekamilisha ujenzi wa zahanati katika Kijiji cha Kafisha Kata ya Ikola na I kiwe imeanza kufanya kazi ifikapo Agosti 30 iliianze kutowa huduma kwa wananchi wanao ishi mwambao mwa ziwa Tanganyika .
Pia waliiagiza Halmashauri hiyo kutowa fedha kwa ajiri ya kiwanda cha kusindika mafuta ya alizeti na karanga cha Mpadeco vinginevyo kama haiwezi kufanya hivyo ikifunge kiwanda hicho kwani akina faida kwa Halmashauri ya Wilaya ya Mpanda na kwa wananchi kutokana na kuwa na mtaji mdogo wa kukiendesha .
Mwenyekiti huyo wa CCM wa Wilaya alieleza kwa upande wa Manispaa ya Mpanda kikao hicho kimeigiza Manispaa hiyo kuhakikisha inakamilisha ujenzi wa sikimu ya umwagiliaji ya Mwamkulu iwe imekamilika ifikapo mwezi Novemba mwaka huu.
Alisema sikimu hiyo ambayo ilipaswa kuwa imeanza kutumiwa na wakulima wa mpunga imeshindwa kukamilika kwa muda mrefu sasa kutokana na uzembe wa mkandarasi hivyo chama hakiko tayari kuona wananchi wanaendelea kukosa huduma hiyo kwa ajiri ya uzembe wa mkandarasi .
Tamko jingine walilolitowa kwa Manispaa wameigiza ikamilishe ujenzi wa ZAhanati katika Kijiji cha Mwamkuru ifikapo mwezi wa nane ambapo inajengwa kwa nguvuya wananchi na Fedha za kutoka Tasaf ambapo wananchi walisha kamilisha mchango wao zilizobaki ni fedha za kutoka Tasaf.
0 comments:
Post a Comment