Home » » WAPEWA SEMINA YA SHERIA MPYA YA UNUNUZI WAUMMA

WAPEWA SEMINA YA SHERIA MPYA YA UNUNUZI WAUMMA


Na  Walter  Mguluchuma
Katavi
Mamlaka ya Rufaa ya Zabuni za  Umma (PPAA)  imetowa mafunzo   ya  uelimishaji  kuhusu  Sheria  mpya ya  ununuzi  wa Umma   na  taratibu  ya uwasilishaji  wa malalamiko  kama  zilivyo ainishwa  katika  sheria  mpya  ya ununuzi  wa  Umma  ya mwaka 2011 kwa wajumbe  wa Bodi za zabuni  Maafisa  ugavi  wa Mkoa wa katavi  na Halmashauri zote za Mkoa wa Katavi   makandarasi na wazabuni
Semina hiyo   ya siku mbili ilifunguliwa hapo jana na Mkuu wa Mkoa wa Katavi Dr  Rajabu Rutengwe ambae ameamishiwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Tanga  kwenye ukumbi wa chuo kikuu Huria cha Mkoa  wa Katavi
Katika  hotuba yake ya ufunguzi Dr  Rutengwe  aliwaeleza washiriki wa semina hiyo kuwa  ni vema watambue kwamba  ununuzi wa  umma  ni  moja  kati ya  maeneo  muhimu  katika  utendaji  wa   Serikali kwani  zaidi ya asilimia sabini  ya  bajeti  ya nchi  inagusa manunuzi
Alisema  mafunzo hayo  ni muhimu  kwani yatawasaidia  washiriki hao  kufahamu  sheria mpya ya ununuzi wa  umma  Namba  7 ya mwaka 2011 na  taratibu  za utatuzi  wa migogoro  itokanayo na ununuzi wa Umma
 Alifafanua Serikali imeweka chombo cha Mamlaka  ya Rufaa ya manunuzi ya  Umma (PPAA)  ili  kuweza  kuwasaidia watu wakate rufaa pale ambapo wanapoona haki haija tendeka
Alisema  Mamlala  ya Rufaa  ya Zabuni  za umma  ni chombo  cha  Serikali  chenye dhamana  ya  kupokea na kutatua  migogoro  itokanayo  na  ukiukwaji  wa  taratibu  za ununuzi  wa umma  kama zilivyoanishwa  katika  sheria  ya ununuzi  wa  Umma  ya mwaka 2011
 Dr  Rutengwe  alieleza  lengo kuu la kuanzishwa  kwa mamlaka  hii  ni kuwa chombo  ambacho  kitatatua  migogoro  itokanayo  na ununuzi  wa Umma  nje ya mahakama  ilikutochelewesha  utekelezaji  wa miradi  mbalimbali ya  Serikali  ambayo  ni  muhimu  kwa maendeleo ya Nchi
Kwa upande wake mwanashria wa PPAA  Florida   Mapunda   aliwaeleza washiriki wa semina hiyo kuwa sheria  hiyo Mpya namba 7  ya manunuzi ya umma ya mwaka 2011 imanza kutumika Desemba  20 mwaka jana 
 Alisema  kabla ya mwaka  2001  Tanzania  haikuwa  na  mfumo  rasmi wa  sheria  wa ununuzi wa Umma  wala   chombo  mahsusi  cha kudhibiti  hivyo mfumo  na taratibu  za ununnuzi wa umma  zilitofautiana  na  hazikuwepo  taratibu  maalumu za  uwajibikaji
Aliwafafanuliwa washiriki hao kuwa  mpaka sasa  mamlaka hiyo ya Rufaa ya manunuzi za umma imeisha pokea kesi za rufaa miambili na arobaini
 Nae   Kaimu   katibu mkuu wa (PPAA) Mbile Kissiok  alisema kuwekupo na malalamiko mingi ya watu  wanaokuwa wameomba tenda mbalimbali  kutokana  na  kutofahamishwa  kwa matokeo  ya tenda  wanazokuwa wameomba
 Alisema ni wajibu kwa maafisa ununuzi  kuwapatia taarifa ya matokeo ya mshindi wa  tenda hata kama  aliyeomba tenda anapokuwa ameshindwa  badala ya kutoa taarifa kwa mtu  aliyeshinda tenda tuu

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Katavi yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa