Home » » MWANAFUNZI AJIUWA BAADA YA KUFELI MTIHANI WA DARASA LA SABA

MWANAFUNZI AJIUWA BAADA YA KUFELI MTIHANI WA DARASA LA SABA

 Na Walter wa Katavi yetu
MWANAFUNZI, Jenifa Leonard (17) aliyekuwa akisoma katika shule ya Msingi Shanwe, Halmashauri ya Mji wa Mpanda,  amejiuwa kikatili baada ya kubaini kuwa  amefeli  mtihani  wa kumaliza elimu ya msingi  mwaka huu .
Habari kutoka  eneo la tukio zimebainisha  kuwa marehermu alikunywa  dawa za aina mbalimbali  akitumia mafuta ya taa baada ya kukasilishwa na matokeo yake ya kufeli mtihani wa darasa la saba.
Kwa mujibu  wa akaka yake , Masumbuko Leonard  , marehermu alifariki usiku wa kuamkia jana majira ya saa nane na nusu usiku muda mfupi baada ya kufikishwa katika Hospital ya Wilaya ya Mpanda kwa  matibabu
Alisema siku hiyo ya tukio marehemu  ambae  amemaliza darasa  la saba mwaka huu Katika Shule ya Msingi Shanwe  pamoja na mdogo wake aitwaye  Jackilina Wiliamu  walikuwa wamekaa nyumbani  ndipo walipoletewa taatifa ya  matokeo ya darasa la saba na mwanafunzi waliemaliza nae shule moja .
 Alisema   mwanafunzi huyo  alimweleza marehemu  na mdogo wake kuwa  matokeo ya ufaulu wa darasa  la saba yaliotangazwa  na Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi  yameonyesha kuwa  marehemu amefeli    ila mdogo wake  Jackilina yeye amefaulu mtihani huo.
Baada ya kuambiwa hivyo marehemu hakuamini aliamua kwenda kwenye mtandaa ili aweze kuhakikisha kama kweli amefeli mtihani wa kumaliza darasa la saba  na alifika  huko alikuta matokeo ni kama alivyokuwa ameambiwa ya kuwa amefali
 Alieleza marehemu  Jenifa kisha alirudi nyumbani na kumkuta mdogo wake  ambae yeye amefaulu na alimweleza  kuwa anaona aibu yeye mkubwa kufeli  na mdogo wake  amefaulu hivyo ni bora anywe sumu
 Alisema  aliendelea kumweleza mdogo wake  kuwa anamtakia  aendelee na masomo vizuri  na maisha ya hapa duniani  kwani yeye na mdogo wake hawata onana tena Dunia kwani yeye anatangulia mbele za haki
Masumbuku alieleza kisha marehemu aliingia ndani ya chumba  cha mama yake aitwaye  Stela Joseph ambae muda huo hakuwepo nyumbani  na ndani ya chumba hicho kulikuwa na dawa za binadamu za aina mbalimbali ndipo  alipozichukuwa na kuzinywa kwa kutumia mafuta ya taa
 Alisema kisha alitoka sebuleni na kumkuta  Jackilina na  alimweleza kuwa tayari ameisha kunywa  dawa  kwa kutumia mafuta kutokana na kukasilishwa na matokeo yake ya darasa la saba hata hivyo Jackilina  alifikiri  dada yake anamtania
“ Baada ya muda marehemu alianguka chini   na kumfanya  Jackilina akote nje na kukimbia kwenda kuomba msaada  kwa majirani  ambao walimkimbiza katika Hospitali  ya  Wilaya ya Mpanda   hata hivyo ilipofikia majira ya saa nane na nusu usiku akafariki dunia
 mwili wa marehemu umehifadhiwa katikachumba cha kuifadhi maiti katika Hospitali ya Wilaya ya Mpanda na mazishi yanatarajiwa kufanyika leo katika  makaburi ya Shanwe ‘ alibanisha

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Katavi Dhahiri Kidavashi  amethibisha kutokea  kifo cha mwanafuzi huyo na  jeshi la polisi  linaendelea na uchunguzi zaidi kuhusiana na kifo hicho
Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Katavi yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa