Na Walter ,.Mguluchuma
Katavi
Muhuga alisema hayo jana baada ya kupokea taarifa ya Afsa Mipango wa Halmashauri ya wilaya ya Mlele Seif Mohamed Makome kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika katika kijiji cha Mkuyuni Kata ya MajiMoto ndani ya ziara maalumu ya siku mbili aliyoifanya Wilayani humo.
Ziara hiyo ilikuwa na lengo mahususi ya kujitambulisha kwa Wananchi,Mkuu wa mkoa huyo baada ya kuteuliwa na rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tazania Dk John Magufuri ikiwa pamoja na kukagua ujenzi wa miradi mbalimbali iliyo kamilika ya Maji safi na salama Kata ya Mamba iliyo gharimu T sh 2,199,653,981/=,Machinjio ya kisasa ya Mifugo kata ya MajiMoto Tsh115,538,082/=,Mghara mawili ya kuhifadhi mazao katika kijiji cha Mwamapuli Tsh 250,000,000/=.
Aidha,Ukarabati wa Nyumba ya Afsa mtendaji wa kata ya Usevya kwa ajili ya Ofsi za Muda Mfupi za Halmashauri Mpya ya Mpimbwe ulio gharimu Tsh 35,214,150/= Ikiwa pamoja na ujenzi wa Zahanati na Nyumba moja ya Mtumishi Tsh 22,300,400/=,Ambapo miradi yote hiyo imejengwa katika Halmashauri ya Mpimbwe Wilayani Mlele.
Mkuu wa Mkoa alisema uingizwaji wa mifugo katika hifadhi ya Katavi unaleta sura mabaya kwa Mkoa,Ambapo athari zake ni kubwa sio tu katika uharibifu wa Mazingira bali unaweza kusababisha mlipuko wa magonjwa hifadhini.Hivyo kuhatarisha baadhi ya Wanyama kutoweka na kupoteza vivutia vya Watalii.
''Ndugu Wafugaji tambue kuwa Serikali haiwezi kuwafumbia macho Wafugaji wanaoingiza Mifugo kwenye hifadhi ya Taifa na kupitia sheria ya mwaka 2009 inayosema Mifugo yoyote itakayo ingia ndani ya hifadhi ya Taifa itakamatwa na kutaifishwa''Alisema.
Aliongeza kuwa Ufugaji wa Mifugo mingi usio wa kisasa hauna tija yoyote,Hivyo Wafugaji inawapasa kuuza Mifugo yao na kujenga Nyumba bora za makazi na biashara.
''Wafugaji wote,Kupitia taarifa niliyosomewa.Ndani ya Wilaya ya Mlele kuna jumla ya zaidi ya Mifugo Laki nane ni jambo jema mkaimarisha uchumi wenu kupitia mifugo hiyo kwa kutumia machinjio ya kisasa yaliyo jengwa katika kata ya MajiMoto.Kwani mtaweza kupata Nyama safi,Ngoza bora ikiwa pamoja Kwato na Pembe mtakazo nje ya Nchi''Alisema.
Sanjali na hayo Muhuga aliwaambia Serikali haina nia mbaya na Wafugaji wote kwa kutambua mchango wao katika ukuzaji wa uchumi nchini.Hivyo inafanya juhudi ya kuweza kutafuta eneo maalumu kwa ajili ya kulishia mifugo na kuondoa migogoro kati ya Wafugaji na Wakulima.
Nao,Mkuu wa Wilaya ya Mlele Issa Njiku na Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya Mpimbwe Erasto Kiwale waliwaambia wafugaji kufuata kanuni na sheria za Taifa,Hasa katika kuzingatia ufugaji wa kisasa ikiwa pamoja na kutokuingiza mifugo ndani ya hifadhi.
Kwa upande wa baadhi ya Wananchi ambao ni Wafugaji na Wakulima walimshukuru Mkuu wa Mkoa Meja Jenerali(mst) Raphael Muhuga kwa ziara yake wilayani humo maana itawapa hamasa ya kufanya kazi kwa bidii na kutekeleza maagizo yake kwa faida ya ustawi wa Taifa la Tazania.
0 comments:
Post a Comment