Home » » TUMBAKU ZAIDI YA KILO MILIONI 9.2 KUZALISHWA MKOANI KATAVI KATIKA MSIMU WA 2015 NA 2016

TUMBAKU ZAIDI YA KILO MILIONI 9.2 KUZALISHWA MKOANI KATAVI KATIKA MSIMU WA 2015 NA 2016

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 



  Walter  Mguluchuma
         Katavi
Wakulima wa  vyama   vya  ushirika   wa   Tumbaku  katika Mkoa wa  Katavi wanatarajia kuzalisha na kuuza  zaidi ya kilo  Milioni 9.2 za  Tumbaku  katika  msimu wa kilimo wa 2015 na 2016  uzalishaji huo ukiwa umeshuka  kiwango cha asilimia 22 ya uzalishaji  wa  msimu uliopita wa 2014 na 2015 ambapo zilizalishwa na kuuzwa kilo Milioni 11.9.
Hayo yalisemwa  hapo  juzi  katika  risala  ya Wakulima wa Tumbaku  wa  Mkoa wa Katavi  iliyosomwa   na  Mwenyekiti  wa  Chama  kikuu cha ushirika cha  Wakulima wa Tumbaku Mkoa wa  Katavi  LATCU    Modesti  Yamlinga   mbele ya  mgeni  rasmi  Mkuu wa Mkoa wa  Katavi  Meja  Jenelali  Mstaafu  Raphael  Muhuga wakati  wa   sherehe za uzinduzi  wa masoko  ya ununuzi wa Tumbaku  wa  msimu wa 2015 na  2016  zilizofanyika  katika  Kijiji  cha Igagala    chama  cha Msingi  Mpandakati .
Yamlinga  alisema  katika  msimu  huu wa 2015 na 2016 Wakulima  wa vyama vya ushirika wa  Tumbaku wanatarajia kuzalisha  na kuuza Tumbaku  yenye  jumla ya Kilo 9,265,796 ukiwa umeshuka kwa asilia  22.21 ukilinganisha na uzalishaji wa msimu wa kilimo uliopita wa 2014 na 2015 ambapo uzalishaji    wa  Tumbaku ulikuwa ni kilo 11,910,459.
 Alieleza kuwa bei ya Tumbaku  huwa inapangwa mapema na Tobacco Council kabla ya  msimu  hauja   anza   hivyo  mkulima  huwa   anakuwa  na uhakika  na bei  ya kuuzia   zao  lao mapema .
Katika  sekta ya  Tumbaku wamejiwekea  utaratibu  wa kufuata  kanuni  za kilimo  cha Tumbaku  kwa kila mkulima kupanda miti  na kila  Chama  cha ushirika  cha msingi kinatakiwa  kiwe na  shamba  la miti  ikiwa  ni pamoja na kutunza  miti ya asili.
Mwenyekiti  huyo wa   Latcu alisema  katika  vipindi hivyo viwili vya  msimu wa 2014 hadi  2016 Wakulima wa  vyama  vya  msingi vya ushirika wa  Wakulima wa Tumbaku wameweza  kupanda   hadi sasa   miche ya  miti 8,919,206.
Alivitaja  vyama  vya  Msingi  saba  vya Wakulima  wakulima wa Tumbaku vilivyoko  katika  Mkoa wa Katavi  kuwa ni  Ilunde,Ukonongo,Katumba ,  Nsimbo ,  Mpandakati , Kasokola  na  Mishamo na Makampuni  yanayonunua  Tumbaku  Mkoani  hapa  ni  TLTC  na   Premium.
 Baadhi ya   changamoto  zinazo  wakabili wakulima wa Tumbaku  alizitaja kuwa ni  ubovu wa  barabara katika  maeneo yanayozalisha Tumbu na  wakulima  kutokuwa waaminifu kwa  kuwauzia watu tumbaku yao ambao sio wakulima hari ambayo imefanya baadhi ya wakulima kushindwa kulipa madeni yao .
 Changamoto  nyingine  ni  uchomaji  holela wa moto  kwenye  mashamba ya miti  unaofanywa  na raia wengine pamoja  na uchache wa Makampuni yanayonunua Tumbaku  hari inayosababisha kutokuwepo kwa ushindani wa biashara.
Kwa  Upande  wake  Mkuu wa  Mkoa  wa  Katavi  aliwataka   viongozi  wa  vyama vya Msingi  wasimamie  majukumu yao  kikamilifu  ili wakulima wao  waweze  kupata  malipo  sitahiki.
 Alisema  wapo  viongozi na wanachama  wanao  saliti  ushirika  ni vizuri  mkawashughulikia  haraka  kwa mujibu wa  sheria  ili  kuunusuru ushirika wa zao la  Tumbaku  kwa  ujumla  wake .
Meja  jenelali  Muhuga  aliwataka  viongozi wa vyama vya  Msingi  kuhakikisha  wanaandaa  orodha  sahihi  ya wanachama  na wasio wanachama ,kwani wanaosadikiwa  kuleta  vurugu  kwenye  vyama vya msingi  vya ushirika  wengi wao  si wanachama   wa  vyama vyao  na hao  ndio  wanauwezo wa kuweka  maazimio  mabovu .
Tekelezeni  hilo  na  nipate  taarifa   kabla  ya  masoko  ya  Tumbaku   ya  msimu  huu niliyofungua  hajafikia mwisho alisema   Meja  Jenelali Mstaafu Raphael  Muhuga .
Nae  Mkuu wa Wilaya  ya  Mpanda  Paza  Mwamlima  alisema  zao  la  Tumbku  ndio zao  mama  katika  Mkoa wa Katavi  ambalo linamwingizia  pesa  mkulima  kuliko  mazao  mengine .
 Hivyo  wanaushirika wa  Tumbaku wasikubali kuuwa ushirika wao  kwani  ndio  umekuwa mkombozi wa kuwasaidia watu  wa kipato cha  chini .

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Katavi yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa