Home » » Wanawake na wasichana wanaofanya biashara katika masoko ya Manispaa ya Mpanda wamepatiwa mafunzo ya kukuza sauti

Wanawake na wasichana wanaofanya biashara katika masoko ya Manispaa ya Mpanda wamepatiwa mafunzo ya kukuza sauti

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 
   

Na   Walter    Mguluchuma
                Katavi  yetu blog
Wanawake na wasichana wanaofanya biashara   katika   masoko ya      Manispaa ya Mpanda   wamepatiwa  mafunzo  ya kukuza  sauti  na kuimarisha  haki za    mwanamke  na  wasichana  kushiriki   nafasi  za uongozi  katika  maeneo  ya masoko wanakofanyia  kazi  na wanako ishi .
Mafunzo  hayo ya  siku  moja  yaliyoandaliwa  na  shirika  la   Tanzania  Community Media  organization TACOMO yalifanyika  jana  katika  ukumbi wa  Mtakatifu  Maria Mjini  Mpanda.
 Kiongozi  mkuu wa  shirika  hilo lisilo la  Kiserikali  lenye   makao yake  makuu  Jijini  Mbeya  Gordon   Kalulunga  alisema     mafunzo  hayo  yanalengo la kuwaelimisha wanawake  na wasichana  watambue  haki yao  ya  kuwania uongozi  katika   sehemu zao wanazofanyia kazi na  wanako ishi  pia walipatiwa mafunzo  ya ujasilimali kwa wanawake .
Alisema   wanawake  wamekuwa  hawajitokezi kuwania  nafasi mbalimbali kwenye  maeneo wanayofanyia kazi na wanako  ishi kutokana  na kuwa waoga wakati uongozi ni  kalama  ndio   maana  TACOMO imeamua  kutowa  mafunzo  hayo ili wanawake  na  wasichana  watambue  haki yao ya kuwania uongozi  katika  sehemu zao wanazofanyia kazi na wanako ishi .
  Afisa Maendeleo jamii wa Kata za  Kashaulili na Majengo  Imelda  Mkama  alieleza  kuwa  mafunzo  hayo waliopatiwa   wanawake   na  wasichana  yatawafanya  ushiriki wa  wanawake  kuwa  mkubwa  katika kuwania  nafasi mbalimbali za uongozi .
Kuhusu  ujasilimali  afisa  huyo wa  Maendeleo ya  jamii   alieleza  kuwa  mjasilamali   lazima  awe ni  mtu  ambae  si wakukata tama na awe ni mtu mbunifu wa shughuli  za  kufanya  na  asiwe mtu wa kuiga biashara ya mtu mwingine.
Salome  Mwanandeje  mshiriki wa  mafunzo hayo  alisema  wanawake  wengi wamekuwa  hawajitokezi kuwania  nafasi za uongozi  kwa kuwa huwa wanajihisi kuwa  wakigommbea  watashindwa wakati wanawake wanaweza.
 Alisema wanawake  wamekuwa  hawagombei kwa  wingi nafasi za uongozi kwa kuwa  huwa  awajiamini  na pia wamekuwa  hawapendani wao kwa wao badala ya kutiana  moyo wamekuwa wakikatishana tama.
Juliana  Nyanda alisema  elimu kwa jamii bado  ipo chini  kwenye uelewa  wa kugombea  nafasi  mbalimbali   za uongozi  kwa  wanawake .
Nae  Asha  Tende alieleza kuwa wamekuwa wakikatishwa tama kugombea   nafasi za uongozi  kutokana na baadhi ya  makabila  yamekuwa na   tabia hayataki  kutawaliwa  na wanawake.
Washiriki wa  mafunzo  hayo ya siku  moja yalwashirikisha  wanawake  na wasichana wanaofanya  biashara  katika  masoko ya Buzogwe,  Mpandahotel, Makanyagio, Soko kuu na  soko la matunda la  Kawajense yalioko   katika  Manispaa ya Mpanda.

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Katavi yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa