Walter Mguluchuma na Irine Temu
Katavi yetu Blog
Mahakama ya Wilaya ya Mpanda Mkoa wa Katavi imemuhukumu Kasanzu Kwimba Mkazi wa Kijiji cha Maduu Wilaya ya Mlele kifungo cha miaka 20 jela baada ya kupatikana na hatia ya kupatikana na nyara za Serikali zenye thamani ya zaidi ya Shilingi Milioni 15.
Hukumu hiyo ilitolewa jana na Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya Wilaya ya Mpanda Chiganga Ntengwa baada ya kulidhika na ushahidi uliotolewa Mahakamani hapo na upande wa mashitaka .
Awali katika kesi hiyo Mwanasheria wa Mkoa wa Katavi Jamila Mziray alidai Mahakamani hapo kuwa mthumiwa alitenda kosa hilo hapo mei 27 mwaka jana katika Kijiji cha Maduu Wilaya Mlele.
Alidai kuwa siku hiyo ya tukio mtuhumiwa alikamatwa nyumbani kwake akiwa na nyara mbalimbali za Serikali akiwa amezihifadhi ndani ya nyumba yake zenye thamani ya shilingi Milioni kumi na tano na laki saba .
Mziray alizitaja Mahakamani hapo nyara alizokamatwa nazo mthumiwa kuwa ni ngozi ya chui moja , ngozi ya Simba samba moja ngozi ya nyumbo moja na ngozi paka pori .
Mwanasheria huyo aliiambia Mahakama kuwa mtuhumiwa alikamatwa baada ya jeshi la polisi na askari wa Hifadhi ya Taaifa ya Katavi kupata taarifa kuwa mtuhumiwa anamiliki nyara za Serikali kinyume cha sheria na ndipo walipomfanyia upekuzi waliweza kumkuta na nyara hizo za Serikali.
Hakimu Mkazi Mfawidhi Chigamga Ntengwa akisoma hukumu hiyo aliieleza kuwa kutoka na ushahidi uliotolewa Mahakamani hapo Mahakama imeridhika na ushahidi uliotolewa mahakamani ambapo mshitakiwa amepatikana na hatia.
Alieleza kkutokana na kupatikana na kosa hilo mahakama inatowa adhabu kwa mshitakiwa ya kifungu cha sheria Namba 235 ya marekebisho ya sheria ya mwaka 2002.
Hivyo Mahakama imemuhukumu Kasanzu Maduu kutumikia kifungo cha miaka ishirini jela kuanzia jana ili ikaweze kuwa na tabia njema akimaliza kifungo chake kwenye jamii
0 comments:
Post a Comment