Home » » WANAOZUIA ASKARI KUTEKELEZA MAJUKUMU YAO WACHUKULIWE HATUA KALI

WANAOZUIA ASKARI KUTEKELEZA MAJUKUMU YAO WACHUKULIWE HATUA KALI

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 

Na Walter Mguluchuma
Katavi

MWENYEKITI wa kamati ya ulinzi na usalama wa wilaya ya Mlele mkoani Katavi Said Njiku ameliagiza jeshi la polisi wilayani humo kuwakamata na kuwafikisha mahakamani baadhi ya wakazi wa kijiji cha Kasansa ambao wanatuhumiwa kuwazuia askari polisi kutekeleza majukumu yao.


Mkuu huyo wa wilaya alitoa agizo hilo jana baada ya askari polisi wa kituo cha Majimoto wilayani humo kushambuliwa kwa mawe na wananchi wakati wakienda kumkamata mganga mmoja wa jadi maarufu kwa jina la kamchape ambae wananchi hao walikuwa wamemwita kijijini hapo ili awaondoe uchawi watu waliokuwa wakidaiwa kuwa ni wachawi.


Siku ya Mei 13 majira ya saa 8 za mchana  polisi walipata taarifa za siri kutoka kwa mmoja wa wakazi hao walifika katika kijiji hicho ili kumkamata kamchape huyo ambaye alikuwa anafanya kazi ya kuwanywesha dawa watu waliokuwa wakituhumiwa kuwa ni wachawi ili waache kuroga.


Akiwa anaendelea na kazi hiyo ghafla gari la polisi lilifika kijijini hapo hali iliyowaudhi wananchi wakijua kuwa polisi wamefika kuzuia zoezi hilo ndipo walipochukua mawe na kuanza kuwarushia polisi hao ambao walikuwa wameongozana na mwananchi aliyewapa taarifa hali iliyosababisha polisi hao kuzidiwa nguvu na kukimbilia katika ofisi ya kata.


Wananchi hao wakiwa wamejaa jazba walifika katika ofisi hizo na kupasua vioo kwa mawe na kisha kuvunja mlango kitendo kilicho sababisha polisi wakimbie na kisha kumpiga mwananchi aliyekwenda kutoa taarifa polisi na kumjeruhi vibaya ambapo amelazwa hospitalini anapatiwa matibabu.


Kutokana na tukuio hilo ndipo mwenyekiti huyo wa ulinzi na usalama alipofika kijijini hapo na kuitisha mkutano wa hadhara na kukemea kitendo hicho na kuwaagiza polisi kuhakikisha wanawasaka watu wote waliohusika na vurugu hizo ili sheria ichukue mkondo wake.


Baadhi ya wakazi wa kijiji hicho ambao wengi wao ni wanaume wamekimbia nyumba zao pamoja na huyo kamchape ambapo wanaishi porini wakihofia  kukamatwa na polisi kutokana na maagizo aliyotoa mkuu huyo wa wilaya.

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Katavi yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa