Home » » DIWANI WA CCM KIZIMBANI KWA RUSHWA YA TSH 400,000 ZA MFUGAJI WA MIFUGO

DIWANI WA CCM KIZIMBANI KWA RUSHWA YA TSH 400,000 ZA MFUGAJI WA MIFUGO

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 


    Na  Walter  Mguluchuma
   Katavi

 TAASISI   ya kuzuia   na  Kupambana  na  Rushwa   TAKUKURU     Mkoa  wa  Katavi  imempandisha  kizimbani   katika  Mahakama  ya  Wilaya  ya  Mpanda  Diwani wa  Kata  ya  Katumba     Tarafa  ya  Nsimbo  Wilaya  ya  Mlele    Senator  Baraka   Jerith  kwa  tuhuma  za kushawishi na kupokea  Rushwa kiasi  cha  Tsh  400,000  kutoka  kwa  mfugaji wa  Ng-ombe.
  Mhumiwa  huyo   alifikishwa   kizimbani   hapo  jana   mbele ya  Hakimu  Mkazi   Mfawidhi wa  Mahakama  ya  Wilaya ya  Mpanda  Chiganga  Ntengwa  na  kusomewa  mashitaka  na  wanasheria wa TAKUKURU  Mkoa  wa  Katavi   Simon  Buchwa  na  Bahati  Haule.
Mtuhumiwa  anadaiwa  kutenda  makosa  hayo  mawili   hapo   mnamo  tarehe   12  Mei  mwaka huu  katika  mgawaha wa   mtu  mmoja  aliyejulikana kwa jina  moja la    Ngandieta  huko  katika  Makazi ya  wakimbizi ya  Katumba  kinyume  na  kifungu  cha  sheria   15 kidogo cha kwanza  b cha  sheria  ya kudhibiti  na  kupambana na  Rushwa   Na 11 ya  Mwaka  2011.
Siku  hiyo  mshitakiwa  Diwani   alipokea kiasi cha  shilingi   laki  nne  kutoka  kwa   Mfugaji wa  Ng-ombe  anaitwa  Charles  Msukuma   ili  amsaidie kutohamisha  mifugo yake kwenye  eneo  tengefu  la  makazi ya wakimbizi ya  Katumba  iwapo  angekubali kumpatia kiasi cha  shilingi milioni  moja  ili  asitekeleze  amri  iliyotolewa  na  Mahakama ya  mwanzo  Katumba ya kumtaka  mchungaji  huyo kuondoa mifugo kwenye  eneo hilo.
Wanasheria  hao wa  TAKUKURU  walidai  mahakamani  hapo  kuwa  mshitakiwa  katika   shitaka  la kwanza  anatuhumiwa  kwa  kosa  la kushawishi  kwa nia ya kupokea  Rushwa  kifungu  cha 15  kidogo cha kwanza b  cha  sheria  ya kupambana  na  Rushwa  Namba  11  cha  mwaka  2011   sheria jambo  ambalo ni  kinyume  cha  sheria .

Shitaka  la  pili  ameshitakiwa kwa kosa  la pokea  Rushwa  kiasi cha  shilingi  laki  nne   kinyume  na  sheria  ambapo  mshitakiwa  baada ya  kusomewa  mashitaka  hayo  mawili  alikana .
  Mwanasheria  wa  TAKUKURU  Simon  Buchwa   aliiomba   Mahakama ipange  tarehe  nyingine ya kesi hiyo kwa  ajiri ya kutajwa kwa kuwa  upelelezi wa kesi hiyo hauja  kamilika   .
Hakimu  Mkazi  Chiganga  Ntengwa  aliharisha  kesi hiyo hadi Mei  30  na  mshitakiwa  alikwenda  rumande  baada ya kushindwa kutimiza  masharti ya  mdhamana  ambapo  alitakiwa kuwasilisha kiasi cha  shilingi  milioni mbili keshi mahakamani  hapo au mali yoyote  isiyo hamishika .
 Mshitakiwa huyo ni miongoni mwa waliokuwa  Raia wa  Nchi ya  Burundi  ambao  Serikali  iliwapatia  Urai  wa  Tanzania  hivi  karibuni

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Katavi yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa