Home » » BIASHARA YA AKINA DADA POA YASHIMILI MPANDA WAKODI NYUMBA MBILI ZA KULALA WAGENI

BIASHARA YA AKINA DADA POA YASHIMILI MPANDA WAKODI NYUMBA MBILI ZA KULALA WAGENI

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 

      Na    Walter  Mguluchuma
               Katavi
Baadhi ya  Wakazi wa  Mji wa  Mpanda Mkoa wa  Katavi  wengi wao wakiwa ni   Wanafunzi wa kiume   katika  Shule za  Msingi  na  Sekondari   wako  katika  hatari  kubwa  ya kupata magonjwa   mbalimbali yatokayo  na  Ngono  ukiwemo Ukimwi baada  ya kushamiri  kwa  biashara  ya kuuza  miili   kufutia  kundi kubwa  la  madada  poa  kuvamia   Mji wa   Mpanda  na kukodi  nyumba  mbili za kulala wageni  na kisha kufanya biashara ya kujiuza  kwa bei ya kuanzia   shilingi 2000 huku wateja wao wakubwa wakiwa ni wanafunzi wa Sekondari na  shule za Msingi.
Biashara  hiyo ya   ngano  imeshamiri zaidi   katika  Mtaa wa  Majengo  B  ambao  unajulikana kwa  jina  la  maarufu kuwa ni  Mtaa wa  FISI   baada ya  akina  Dada  poa  kuhama  katika    mikoa   mingine na  kuhamia  Wilayani  Mpanda   huku  wengi wao wakiwa wanatoka  katika  Mikoa ya  Mwanza, Mbeya  na   Kigoma.
Dada  poa  hao  ambao  wamegundua  mbinu  mpya badala ya kukaa kwenye  madanguro wao  wameamua  kukodi  nyumba  mbili za  kulala  wageni  ambazo  zipo  jirani  jirani  katika Mtaa huo  ambazo  majina zake  tuunayo   kwa  ajiri ya kufanya  biashara  hiyo ya  Ngano .
Gazeti  hili lilizungukia  juzi  kwenye  eneo  hilo  baada  ya kupokea  malalamiko  kutoka  kwa  wakazi wa  mtaa huo  lilishuhudia  makundi  makubwa ya  vijana  wakiwa  wamepanga  foleni  kwa ajiri  kuingia   ndani ya  nyumba hizo za kulala  wageni huku   baadhi ya  akina  dada poa  hao wakiwa  wanalandalanda na wamevaa nguo zisizo za  heshima.
 Akizungumza   na  gazeti  hili   mmiliki  mmoja  wa  Bar inayouza  vinywaji  vikari  alisema   biashara  hiyo   imekuwa  ikifanyika  zaidi  kuanzia  saa   moja ya  usiku   hadi     saa  sita  usiku .
Mmoja  wa  dada  poa hao  akizungumza  na  gazeti  hili   akiwa  kwenye   bar  ya  Zebra ilipo  kwenye  mtaa huo  ambae  yeye  alijitambulisha   kuwa  ni  mkazi wa  kutoka  Mkoa wa  Mwanza  alisema  yeye  na  wenzake waliamua  kuacha  kuishi  kwenye  nyumba za  danguro baada ya kuona wa wakikamatwa  mara  kwa  mara  wakati wa  misako ya  polisi  .
  Alisema  toka  walipoamua  kukodi   nyumba  hizo  mbili  za  kulala  wageni  wameacha kusumbuliwa  na  misako ya mara kwa  mara  na wamekuwa  wakifanya  biashara  hiyo kwa uhuru  tofauti  na wakati  walipo kuwa  wanaishi  kwenye  madanguro.
  Alieleza  kutokana  na  biashara  hiyo ya  ngono  wamekuwa     ni sehemu ya  watu wanao  changia  kodi ya  Serikali
  kwani   fedha  wanazomlipa  mwenye   nyumba ya  kulala  wageni  nae  analipia   kodi  ya  Serikalini   tofauti  na  tulivyokuwa tukiishi kwenye  madanguro hatukuwa  tunachangia   kodi  ya  seriakali.
Alifafanua  kuwa  biashara  hiyo wamekuwa  wakiifanya kwa viwango  tofauti   ambapo  kima  cha  chini wamekua  wakianzia  shilingi  1000  na  kina   cha juu kikekuwa  akizidi  shilingi  10,000 ingawa  wateja  wao wengi ni wale wa  kati ya  shilingi  elfu  mbili  na elfu
Mkazi  wa  Mtaa huo   Osca  Seleman  alieleza kuwa  wamekuwa wakipata kero  kubwa  toka wakinada poa  hao walipohamia kwenye  nyumba  hizo za kulala wageni kutokana na kuzagaa kwa makundi ya vijana.
 Pia  hata  vibaka wamekuwa wakizungukia  sana  kwenye  maeneo hayo  hari  ambayo imekuwa ikiwafanya  walale kwa hofu ya kuogapa kuibiwa mari zao  hasa  simu za  mikononi.

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Katavi yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa