Na Walter Mguluchuma
Katavi
Mahakama ya Wilaya ya Mpanda Mkoa wa Katavi imemuhukumu Mwenyekiti wa Kijiji cha Simbwesa CHADEMA Mabula Gilede 30 kifungo cha miezi sita jela baada ya kupatikana na hatia ya kumpiga na kumjeruhi Daktari wa Zahanati ya Simbesa Wilaya ya Mpanda baada ya kumtuhumu kuwa anatibu wagonjwa kwa upendeleo.
Hukumu hiyo ilitolewa hapo jana na Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Wilaya ya Mpanda Odila Amwol baada ya mahakama kulidhika na ushahidi uliotolewa mahakamani hapo .
Awali katika kesi hiyo ambayo mwenyekiti huyo wa Kijiji alikuwa akitetewa na wakil Patrick Mwakyusa mwendesha Kulwa Kusekwa alidai kuwa mshitakiwa alitenda kosa hilo hapo Agosti 19 mwaka jana majira ya saa sita mchana katika Zahanati ya Simbwesa.
Siku hiyo ya tukio mhumiwa alidaiwa kwenda kwenye Zahanati hiyo na kumshambuli kwa kumpiga mateke na ngumi mganga wa Zahanati anaitwa Razalo Michael baada ya kumtuhumu kuwa amekuwa akiwatibu wagonjwa kwa upendeleo kwa kuwapendelea kuwatibu wagonjwa ambao ni wafuasi wa CCM na kutowapatia huduma za matibabu wafuasi wa chama chake cha Chadema.
Alidai Mahakamani kuwa siku hiyo ya tukio mtuhumiwa kabla ya kumpiga Daktari huyo ndani ya ofisi yake wakati akiwa anamtibu mgonjwa alidai kuwa Mganga Razaro alikuwa anawatibu vibaya wagonjwa ambao ni wafuasi wa Chadema na siku hiyo alikataa kumtibi mtoto wa rafiki yake aitwaye Milembe Machime ambae ni mfuasi wa chama chake.
Mwendesha mashitaka Kulwa aliiambia Mahakama kitendo hicho cha mshitakiwa kumshambulia daktari wa kumpiga ngumi na mateke kilisababisha wagonjwa waliokuwepo kwenye zahanati huo kushindwa kupatiwa matibabu siki hiyo kutona na kupigwa kwa daktari.
Katika utetezi wake mshitakiwa Mabula aliiambia Mahakama kuwa yeye ndio aliyepingwa na Daktari huyo hadi aliangushwa chini alipo kuwa amekwenda kumhoji daktati huyo kwa nini amekataa kumpatia matibabu mtoto wa rafiki yake.
Hakimu Odira kabla ya kusoma hukumu aliiambia Mahakama kuwa kutokana na mwenendo mzima wa kesi hiyo na ushahidi uliotolewa mahakamani wa upande wa mashitaka mahakama pasipo shaka yoyote imemwona mshitakiwa anayo hatia hivyo kabla ya kutowa adhabu inatowa nafasi kwa mshitakiwa kama anayosababu yoyote ya kuishawishi mahakama ipunguzie adhabu .
Katika utetezi uliotolewa na Mwanasheria wake Patricki Mwakyusa aliomba mahakama impunguzie adhabu kwani mshitakiwa huyo anao wake watatu na watoto 11 pamoja na mama yake mzazi ambao wanamtegemea yeye.
Pia yeye ni mtu anae aminika kwenye jamii na ndio maana walimchagua kuwa mwenyekiti wa Kijiji na vilevile ajawahi kufanya kosa kama hilo .
Baada ya maombi hayo mwendesha mashitaka Kulwa Kusekwa alipinga na kuiomba mahakama itowe adhabu kali ili kukomesha watu kuendelea na tabia hiyo .
Hakimu Odira aliiambia Mahakama wakati akisoma hukumu hiyo kuwa siku za hivi karibuni kumezuka tabia ya watu kuwashambulia na kuwapiga watumishi wa afya na kwa kuwa mshitakiwa ni mwenyekiti wa kijiji ameweza kufanya kosa hilo na inaweza ikawa kishawishi kwa wananch kuwapiga i wa kawaida iendapo mahakama itamwachia huru baada ya kupatikana na hatia
Hivyo Mahakama imemuhukumu Razalo Michael kutumikia jela kifungo cha miezi sita na kama hajaridhika na hukumu hiyo anayo nafasi ya kukata rufaa .
MWISHO

0 comments:
Post a Comment