Home » » WAALIMU WAANDAMANA KWENDA KWA MWAJIRI WAO KUDAI MADAI YAO ZAIDI YA MILIONI MILIONI 12O

WAALIMU WAANDAMANA KWENDA KWA MWAJIRI WAO KUDAI MADAI YAO ZAIDI YA MILIONI MILIONI 12O

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 


  Na  Walter  Mguluchuma
   Katavi
Hari haikuwa  shwari kwa zaidi ya saa moja  hapo juzi katika Ofisi  za  Manispaa Halmashauri ya Mpanda  jengo  ambalo linatumiwa pia na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Katavi baada ya waalimu  zaidi ya 50 washule za Msingi  na  Sekondari   pamoja  na viongozi wa  chama cha  Walimu wa ngazi ya Wilaya  na Mkoa  kuandamana kwenda kwa mwajiri wao wakitaka  walipwe ya madai yao sungu zaidi ya shilingi milioni 120.
Tukio  hilo  la  walimu  hao kuandamana  hadi kwa mwajiri wao  liltokea  jana  majira ya saanne  hari  ambayo ilisababisha  viongozi wa  Manispaa hiyo kuweza kujifisha  hari  ambayo iliwalazimu   walimu hao kuanza kuimba  nyimba kwenye makolido  kwa muda wasaa nzima  wimbo usemao walimu  ni tegemeo la kuleta maendeleo  na kufanya viongozi wa  Mkoa  na  Manispaa kufanya kikao cha  dharula na walimu hao katika  ukumbi wa Manispaa kilichoongozwa  na  Katibu  Tawala  wa Mkoa wa Katavi wa upande wa  utawala  Salumu  Shilingi.
Mwenyekiti wa Chama cha waalimu CWT waMkoa wa Katavi   John  Mshota  aliwasilisha  madai mbalimbali ya  walimu hao ambayo elieleza kuwa yamekuwa ni yamuda  mrefu bila  kupatiwa ufumbuzi .
Mshota  aliyataja  madai hayo  kuwa  kucheleweshewa  kurekebishiwa  mishahara,kutolipwa   fedha  za nauli  za likizo  kuanzia  mwaka   2013 hadi  2015 kiasi  cha  shilingi   milioni  21,848,050 ,kutolipwa  gharama za  masomoni  shilingi milioni   25,369,700.
Madai  mengine  aliyataja  kuwa ni  kutolipwa kwa walimu  wastaafu  za kuwarudisha  kwao  kiasi  cha  shilingi  milioni  23,839.700, gharama za uhamisho  kiasi cha  shilingi  milioni 5,093,000,gharama za  matibabu  shilingi  milioni   23,189,100 na  fedha za   chama  chao  cha  ushirika  wa kuweka  na kukopa   cha MPATE SACCOS      shilingi  milioni  24,000,000.
Mwenyekiti  huyo wa  CWT  Mkoa wa  Katavi  alieleza  kuwa   mwajiri wao ambae ni mkurugenzi wa   Manispaa  ya  Mpanda  ameshindwa kupeleka  michango  wake  kwenye mfuko  wa PSPF  hari  ambayo    imewaathiri  walimu  wanaostaafu  kulipwa malipo yao ya mafao ya kinunua mgongo  kidogo  na kutopewa  hati zao za malipo yao ya  msharahara Salary  Slips za  mwezi  Agosti 2008.
Nae   Katibu wa  Chama  cha  Walimu  Wilaya ya  Mpanda   Wilisoni  Masolwa  alieleza chama cha  Walimu  kilimwandikia barua  mwajiri wao  ya  tarehe  10  machi   2016 na kumpa  siku  10 yaani  hadi  machi 24  awe  ametekeleza  madai hayo lakini  hadi  hiyo juzi  alikuwa  mwajiri wao  hajatekeleza wala kuwajibu majibu ya  barua hiyo kwa maandishi .
Alisema  ndio  maana  waliamua  kuandamana  hadi ofisini  kwa mwajiri  ili  waweze kupatiwa  majibu  ya  madai yao  wanayodai kwa muda  mrefu  sasa  bila kuwepo   dalili za kulipwa  madai  hayo .
Kaimu  Mkurugenzi wa  Manispaa ya  Mpanda  ambae  pia  ni  Afisa  Elimu  Sekondari   Enelia   Lungulu  alikiri  mbele ya  walimu hao kuwepo kwa madai hayo ya walimu.
Alisema  tatizo la kutolipwa kwa walimu hao  halipokwao  bali  tatizo la kucheleweshewa kwa malipo hayo lipo  hazina  ambao  mpaka sasa  hawazituma  fedha za madai ya walimu  kwenye  Manispaa na jitihada za mawasiliano  zinaendelea kufanyika .
Lungulu  alisema  kuhusu  fedha  zao za   MPATE  SACCOS   Kiasi   cha  shilingi  milioni  24  ambazo  zilitumiwa  na  manispaa  hiyo  wanatarajia  kuzilipa  hivi karibuni  kwa  awamu  tatu .
Pia  madai mengine wameshindwa kuyalipa kutokana  na kiasi  kidogo  cha  fedha  zinazoletwa kwa ajiri ya kulipa  walimu za likizo na matibabu .

Afisa  Elimu  wa  Mkoa  wa  Katavi  Ernesti  Hinju alisema  inaonyesha lipo  tatizo baina  ya  manispaa na  walimu  kwenye  swala  la  mawasiliano .
 Alisema  endapo  kungekuwepo na  wasiliano ya  kuwajibu  barua  iliyokuwa imeandikwa na  chama  cha walimu  hata  hari hiyo ya walimu kuandamana isingekuwepo kwa hiyo kuwe  na utaratibu wa kuwepo kwa  mawasilano .
Kabla ya kuanza kikao hicho kilichochukua  saa  nne  Katibu  Tawala wa upande wa  Utumishi alitaka kuwandishi wa habari watoke  ndani ya kikao  hicho  hata  hivyo  walimu hao walikataa na kusema waandishi lazima  wawepo ndani ya kikao hicho.

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Katavi yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa