Na Walter Mguluchuma
Katavi
Mkuu wa Wilaya ya Mpanda Paza Mwamlima amechangisha zaidi ya madawati 200 yenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 13 katika kikao alichokifanya na wadau wa Elimu wa Manispaa ya Mji wa Mpanda.
Kikao hicho cha aliwaeleza wadau wa elimu kwenye
kikao hicho kuwa Wilaya ya Mpanda inakabiliwa na upungufu wa madawati
zaidi ya 13,000 katika shule za msingi na sekondari .
Aliwaeleza Manispaa ya Mpanda inakabiliwa na upungufu wa dawati zaidi ya 5,400na Halimshauri ya Wilaya ya Mpanda zaidi ya dawati 7,700 huku mpaka sasa zaidi ya dawati 2600 zimeisha tengenezwa na kukamilika.
Alisema wilaya ya Mpanda imejiwekea mikakati mbalimbali ya kuhakikisha inakamilisha madati hayo ifikapo mwezi june mwaka huu.
Alizitaja baadhi ya mikakati hiyo ni kila mkuu wa idara kuchangia kiasi cha shilingi laki moja na kila mbao na magogo yanayokamatwa hutaifishwa
na kutengenezwa matofaii pia wameruhusu uvujanaji wa miti ya mbao
kwenye misitu ya Kijiji cha kufuata sheria za mistu.
Mkuu huyo wa Wilaya baada ya kutowa maelezo hayo aliwaomba wadau hao wa Elimu waweze kuchangia fedha au dawati pamoja na vifaa vya kutengenezea madawati .
Wadau hao wa elimu waliitikia wito huo ambapo walichangia jumla ya dawati 224 zenye thamani ya Tsh13,440,000 na fedha kiasi cha shilingi milioni 5,650,000.
Wilaya ya Mpanda imekuwa na kasi kubwa ya ongezeko la wanafunzi waliojiandikisha darasa la kwanza la awali ambapo darasa moja baadhi ya shule wanafunzi wamejiandikisha 800.
0 comments:
Post a Comment