Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Na Walter Mguluchuma
Katavi
Chama cha waalimu CWT Wilaya ya Mpanda Mkoa wa Katavi kimeiomba Serikali kuhakikisha
inawalipa Waalimu wanao
sitaafu malipo yao ya kinua mgongo pindi wanapo sitaarifu kuliko ilivyo
sasa ambapo baadhi ya wasitaafu wamekuwa wakifariki Dunia huku wakiwa
hawajalipwa mafao yao ya kinua mgongo
Hayo lisemwa hapo jana na katibu wa chama cha waalimu Wilaya ya Mpanda Wilson Masolwa mbele ya mwakilishi wa Katibu mkuu wa CWT Taifa Costantine Marcely kwenye risala ya chama hicho aliyoisoma wakati wa sherehe za kuwaaga waalimu waliositaafu kutoka katika Halmashauri za Wilaya ya Mpanda na Halmashauri ya Nsimbo zilizofanyika katika ukumbi wa Kanisa Katoliki Jimbo la Mpana mjini hapa.
Masolwa alisema waalimu wanaositaafu wamekuwa wakikabiliwa na changamoto ya kutolipwa mafao yao ya kinua mgongo kwa wakati pindi wanapokuwa wamesitaafu hali ambayo imekuwa ikipelekea baadhi ya waalimu wasitaafu kufariki Dunia kabla hawaja lipwa mafao yao .
Alieleza kutokana na waalimu wanao kuwa wamesitaafu na kushindwa kulipwa kwa wakati CWT Wilaya ya Mpanda inaiomba Serikari kuhakikisha inawalipa walimu wote wanaokuwa wamestaafu mafao yao kwa wakati .
Risala hiyo ilieleza pia kuwa waalimu wanaokuwa wamestaafu wamekuwa wakikabiliwa pia na changamoto ya kutolipwa fedha za nauri ya kuwarudisha makwao hari ambayo imekuwa ikisababisha wasitaafu waishi maishi ya shida wakati wakiwa wanasubiria fedha za kuwarudisha kwao.
Changamoto nyingine nyinine waliitaja kuwa ni wasitaafu kucheleweshewa kupewa vitambulishi vya Bima ya afya pindi wanapokuwa wamesitaafu wamekuwa haepewi vitambulisho hivyo kwa wakati .
Katika sherehe hizo za kuwapongeza waalimu waliositaafu kumi na moja chama hicho kiliwapatia waliamu waastaafu kila moja bati ishirini ambapo kila msitaafu mmoja alipewa bati zenye thamani ya Ts 340,000 kutoka kwa CWT Wilaya ya Mpanda.
Kwa upande wake mwakilishi wa Katibu mkuu Taifa wa CWT ambae pia ni katibu wa Chama cha waalimu Mkoa wa Katavi Costantine Marcely alisema chama cha waalimu kitaendelea kupigania masilahi ya waalimu .
Alisema kila mwaka jumla ya waalimu 7500 husitaafu hapa nchini na alitoa mfano kuwa ukiona dume la nyani limezeeka ujuwe limekwepa mishale mingi hivyo kwa wataafu hao paka kufikia hatua hiyo wamepitia misuko suko mingi.
Marcely alieza CWT imeisha weka utaratibu kuanzia julai mwaka jana wa kuwazawadia bati 20 wanachama wake wote wan chi nzima wanaokuwa wanastaafu ikiwa ni sehemu ya kuheshimu michango yao walitowa ndani ya chama hicho na mfuko utakapo kuwa mkubwa wataangalia namna ya kuboresha zawadi kwa wastaafu .
Nae mstaafu mwalimu Venansi Nkanga alisema
wakati walipokuwa wanaanza kazi mazingira ya utumishi yalikuwa ni
magumu kuliko ilivyo sasa kwani wakati huo hari ya miundo mbinu ya
barabara ilikuwa ni mibovu .
Alisema kazi ya ualimu ni nzuri ni nzuri pale unapoipenda hivyo aliwaasa waalimu abao bado wanaendelea kufundisha waipende kazi ya ualimu.
Kwaupande wake mstaafu mwalimu Sebastiani Mdula aliwataka waalimu wanaobaki wafanya kazi kwa bidii na nidhamu na kama hawata fanya hivyo wataona kazi ya ualimu ni ngumu.
Mwenyekiti wa chama cha waalimu Mkoa wa Katavi john Mshota aliwataka waalimu kufanya kazi kwa kuzingatia maadili na kuacha tabia ya kutongoza wanafunzi wao wanaowafundisha kwani ni kinyume cha maadili ya utumishi .
Na chama hicho hakitakuwa tayari kumtetea mwanachama wake ambae anavunja maadili ya utumishi kwa makusudi alisema mwenyekiti huyo.

0 comments:
Post a Comment