
Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Na Walter Mguluchuma
Katavi
Mkuu wa Wilaya ya Mpanda Paza Mwamlima ametowa agizo kwa uongozi wa Hospiali ya Wilaya ya Mpanda kuhakikisha inalifungua jingo la wodi la kulaza wagonjwa ambalo limeisha kamilika huku likiwa halitumiki wakati wagonjwa waliolazwa katika hospitali hiyo wanalala wawiliwawili.
Mwamlimu alitowa agizo hilo hapo jana wakati
alipokuwa akizungumza na watumishi wa hospitali hiyo alipokuwa
akizungumza na watumishi hao kwenye hospitali hiyo wakati wa ziara yake
aliyoifanya ya kuangalia changamoto mbalimbali zinazo ikabili hospitali hiyo.
Alisema nijambo la kshangaza kuona wagonjwa katika hospitali hiyo wanalala wawili wawili wakati kuna jingo jipya ambalo limekaa bila kuwa linafanya kazi huku likiwa linaanza kuchakaa.
Aliwatowa agizo ndani ya
siku saba kuanzia jana kwa jingo hilo kuwa limeanza kutumika kwani yeye
hayuko tayari kuona wagonjwa wanalala wawili wawili katika hospitali
hiyo wakati kuna jingo la wodi lipo wazi alifanyi kazi.
Mwamlima pia aliwataka watumishi wa afya kufanya kazi kwa uaminifu mkubwa na kwauadilifu mkubwa katika majukumu yao na wafanye kazi kwa uzalendo zaidi .
Alisema wapo baadhi ya watumishi wa afya wamekuwa wakiwatorea lugha mbaya wagonjwa wakati wakiwa wanawaudumia hivyo hata sita kumchukulia mtumishi yoyote ambaye atakae bainika kufanya hivyo.
Dc huyo alizungumzia kuwepo kwa baadhi ya watumishi ambao sio waaminifu ambao wamekuwa na tabia ya kuwauzia damu wagonjwa wakati damu inatolewa bure.
Alisema madaktari na wauguzi wanapaswa kujitambua kuwa wao ni watu muhimu kwa kuwa shughuli zao zinahusu uhai wa binadamu .
0 comments:
Post a Comment