Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Na Walter
Mguluchuma
Katavi
Mahakama ya
Wilaya ya Mpanda imemuhukumu John Ngasa
(32) Mkazi wa Kijiji cha Mwamkulu Wilaya
ya Mpanda kutumikia jela kifungo cha
miaka mitano jela baada ya kupatikana na
hatia ya kuiba Ng’ombe mbili zenye thamani ya shilingi laki mbili.
Hukumu hiyo
ilitolewa hapo jana na Hakimu mkazi wa
Mahakama ya Wilaya ya Mpanda Odira Amwol mara baada ya kulizika na ushahidi
uliotolewa Mahakamani hapo na upande wa
mashitaka uliokuwa na mashahidi watano.
Awali katika
kesi hiyo Mwendesha Mashitaka
Kulwa Kusekwa alidai kuwa
Ngasa alitenda kosa hilo Aprili 25, 2015 majira ya saa mbili
usiku huko katika Kijiji cha
Mwamkulu Wilayani Mpanda.
Siku hiyo ya tukio mshitakiwa anadaiwa
kukamatwa akiwa ameiba Ng’ombe
wawili wa mwanakijiji mwenzake
aitwaye Madirisha Msalaba zenye thamani ya shilingi laki tisa .
Mwendesha
Mashitaka Kulwa alidai kuwa mtuhumiwa
huyo baada ya kuiba Ng’ombe hao alianza kuwaswaga kwa ajiri ya kuwapeleka eneo
jingine hata hivyo wakati akiwa bado njiani Askari wa jadi(Sungusungu) wa
Kijiji hicho walipata taarifa ya kuibiwa
kwa Ng’ombe hao na ndipo walipofanikiwa kumkamata mshitakiwa Ngasa akiwa
na Ng’ombe hao wawili.
Katika utetezi
wake Ngasa ambae hakuwa na shahidi hata mmoja huku
upande wa mashitaka ukiwa mashahidi watano alikana kuiba Ng’ombe hizo .
Hakimu Odira
Amwol kabla ya kusoma huku aliiambia Mahakama kuwa mshitakiwa amepatikana na hatia ya kuiba
Ng’ombe wawili kutokana na ushahidi
uliotolewa Mahakamani hapo na upande wa mashitaka hivyo mshitakiwa anapewa nafasi ya kujitetea kama unasababu yoyote ya msingi
ya kuiomba Mahakama impunguzie adhabu .
Mshitakiwa Ngasa
katika utetezi wake aliomba Mahakama
impunguzie adhabu kwa kuwa Mama yake mzazi
pamoja na wadogo zake wanamtegemea yeye .
Utetezi huo
ulipigwa vikali na Mwendesha Mashitaka
Kulwa ambae aliiomba Mahakama itowe
adhabu kali kwa mshitakiwa ili iwe
fundisho kwa watu wengine wenye tabia
kama hiyo.
Hakimu Amwol alisoma ukumu na kuiambia Mahakama
kuwa mshitakiwa John Ngasa
amahukumiwa na Mahakama hiyo
kwenda kutumikia jela kifungo cha miaka
mitano jela kuanzia jana na kama haja lidhika na hukumu hiyo anayonafasi ya
kukata rufaa.
0 comments:
Post a Comment