Home » » WAKAMATWA NA MENO YA TEMBO YA MILIONI 120

WAKAMATWA NA MENO YA TEMBO YA MILIONI 120

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 

Na  Walter  Mguluchuma 
  Katavi
Jeshi la Polisi Mkoa wa Katavi linawashikilia watu  watatu kwa tuhuma za kuwakamata na meno ya Tembo yenye thamani ya shilingi milioni 120 ambayo  ni sawa na Tembo wazima wanne .
Watuhumiwa hao watatu waliokamatwa na meno hayo ya Tembo  wametajwa kuwa ni  Bathromeo Agustino(26) Geofrey Exavery(40)  na  Elias Mwelela( 40) wakazi wa Mtaa  wa  Aitel Kata ya Uwanja wa Ndege Manispaa ya Mpansa.
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Katavi Dhahiri Kidavashari aliwaambia waandishi wa Habari jana kuwa watuhumiwa hao walikamatwa  juzi majira ya saa nne usiku katika Mtaa huo wa Airtel waliko kuwa wakiishi.
Alisema    Jeshi  la Polisi  na Askari wa (TANAPA)  wa  HIFADHI  ya Taifa ya mbuga ya Katavi walipatataarifa kutoka kwa Raia wema  kuwa katika Mtaa huo kuna  watu wanamiliki  nyara za Serikali.
Kamanda Kidavashari alieleza   baada ya taarifa hizo kuwa zimepokelewa  na ufuatiliaji  ulifanyika   katika makazi waliokuwa wakiishi watuhumiwa hao watatu.
 Alisema ndipo siku hiyo ya tukio upekuzi ulipofanyika kwenye makazi ya watuhumiwa  na katika upekuzi huo watuhumiwa hao walikutwa na meno ya Tembo vipande 12 vyenye thamani ya shilingi milioni 120  ambayo ni sawa na temba wanne hai yakiwa kwenye makazi yao.
Kidavashari aliendelea kueleza  kuwa watuhumiwa mbali ya kukamatwa na meno hayo ya Tembo pia walikutwa na   mzani mmoja  na Pikipiki aina ya   Sanya  yenye  Namba za usajiriT.552 CZE.
 Alisema  watuhumiwa  wanaendelea  kushikiliwa na  Jeshi la Polisi  kwa hatua za  upelelezi na watafikishwa Mahakamani  baada ya upelelezi  utakapo kuwa umekamilika .
Kamanda wa polisi wa Mkoa wa Katavi ametowa onyo kwa Wananchi kuacha mara moja kujihusisha na biashara  za nyara za Serikali  na biashara haramu .

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Katavi yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa