Home » » WAGANGA WAJADI WACHANGIA KUONGEZEKA KWA UJANGILI KUTOKANA NA KUHITAJI VIUNGO VYA WANYAMAPORI HAO

WAGANGA WAJADI WACHANGIA KUONGEZEKA KWA UJANGILI KUTOKANA NA KUHITAJI VIUNGO VYA WANYAMAPORI HAO

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 

Na  Walter Mguluchuma
Katavi yetu Blog

KUTOKANA na kuongezeka kasi ya waganga wa jadi kutumia viungo vya wanyama pori katika kutoa tiba kumechangia kuongezeka kwa ujangili katika hifadhi ya taifa ya Katavi iliyopo mkoani Katavi.

Baadhi ya wakazi wa mkoa huo wamesema kuwa kitendo cha waganga wa jadi kutumia viungo vya wanyama hao kumesababisha watu wanaopewa masharti ya kutafuta viungo hivyo ili watibiwe kuwinda wanyama hao ili kupata vitu wanavyoagizwa na waganga hao.
Mmoja wa wakazi Hao Fransis Kashamakula akizungumza na mwandishi wa Habari  hii alisema kuwa wakati mwingine wanapokwenda kutibiwa kwa waganga hao wamekuwa wakiambiwa ili wapone ni sharti wapeleke ngozi ya simba ama kwato za swala na hivyo wao kulazimika kutafuta vitu hivyo.

Alisema kuwa niwazi hakuna namna nyingine isipokuwa kuwinda mnyama huyo ili kupata mahitaji hayo ambapo kitendo hicho kinachangia kuua wanyama kutokana na kuagizwa na waganga hao wa jadi.

Alisema watu wengine ni wakulima wa tumbaku mkoani humo ambao wanaamini kuwa waganga wa jadi hutumia viungo vya wanyama hao kama kucha ngozi na vinginevyo kufanya zindiko katika mashamba yao ili wakulima wenzao wasiwaibie mazao yao shambani kwa njia za kishirikina.

Aidha imani nyingine iliyopo ni kuwa waganga hao hutumia vitu hivyo kuzuia mvua ya mawe isinyeshe kwani mvua hivyo inaponyesha shambani mawe huangukia majani ya tumbaku na kuchanika chanika na hivyo kuto faa tena hivyo waganga wamekuwa wakitumia viungo vya wanyama hao ili kufanya zindiko mvua hiyo isiharibu majani hayo ya tumbaku.

Naye Maria Kaswaya mkazi wa mkoa huo alisema kuwa pia kunabaadhi ya magonjwa ya watoto yanatibiwa na waganga hao kwa kutumia ngozi na manyoya ya wanyama hivyo hulazimika kutafuta vitu ambavyo vinaagizwa na waganga hao na hivyo kusababisha kuuawa kwa wanyama katika hifadhi hiyo.

Desemba 27 mwaka jana, mganga wa jadi aliyefahamika kwa jina la Vitus Chomba(42) mkazi wa Sumbawanga mjini mkoani Rukwa alishikiliwa na polisi wa wilaya ya Mlele mkoani Katavi baada ya kukutwa na nyara za serikali ambazo alieleze kuwa huwa anazitumia wakati wa kutibu na kuroga pindi wateja wake wanapohitaji huduma hizo.

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Katavi yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa