Home » » WAPIGWA BUTWAA BAADA YA KUPEWA JENEZA BILA MWILI WA MAREHEMU

WAPIGWA BUTWAA BAADA YA KUPEWA JENEZA BILA MWILI WA MAREHEMU

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 

Na  Walter  Mguluchuma
      Katavi yetu Blog
Waombolezaji waliokuwa kwenye msiba wa  marehemu  aliyekuwa akijulikana kwa jina moja laDanie  uliokuwa katika Mtaa wa Uwanja wa Ndege Mjini Mpanda  katika hari ambayo hawakuitarajiwa  walishikwa na mshituko mkubwa  baada ya  muda wa kumwaga   kabla ya mazishi  baada ya  kufunuliwa sanduku  lililokuwa  linatakiwa kuwemo  mwili  na kukutwa likiwa  na sanduku tupu bila mwili wa marehemu .
Tukio hilo la  aina yake ambalo   lilisimua watu wengi wa Manispaa ya Mpanda  lilitokea hivi karibuni  katika mtaa wa Uwanja wa Ndege .
Siku hiyo ya tukio  waombolezaji hao walikuwa wako msibani katika mtaa huwo wakiwa wanausubilia mwili wa marehemu Daniel   uletwa hapo kwa ajiri ya mazishi ukiwa unatokea chumba cha kuifadhi maiti  katika Hospitali ya Wilaya ya Mpanda  ulikokuwa umehifadhiwa kwa muda wa siku mbili .
Akielezea tukio hilo mmoja wa wanafamili Azack Makanyaga  alisema kuwa  yeye ndiye aliyepewa jukumu na mama mkwe wa marehemu  kushughulikia  taratibu za kuuchukua mwili wa marehemu  katika  chumba cha kuifadhi maiti cha Hospitali ya Wilaya ya Mpanda.
 Alisema alifika kwenye chumba hicho cha kuifadhia maiti huku akiwa  na baadhi ya waombolezaji na wakiwa wamebeba jeneza ambalo waliingia nalo   ndani na kisha walimuacha yeye ndani ya chumba  hicho kwa ajiri ya kuocha  mwili huo wa marehemu .
Makanyaga alieleza  wakati alipokuwa  akiwa anajiandaa kuosha mwili wa marehemu  alitoka  nje ya chumba hicho cha kuhifadhi maiti na kwenda kwenye geti la walinzi na kuwaonyesha kibali cha kuutolea mwili wa marehemu kwenye chumba cha kuifadhi maiti.
Kitendo hicho cha Makanyaga  kwenda kwenye geti la walinzi  kilichochukua muda mrefu  kiliwafanya wale waombolezaji waliokuwa nje ya chumba cha kuifadhi maiti waamue kuingia ndani na kuchukua jeneza wakijua  kuwa mwili wa marehemu  umo ndani ya jeneza  na kisha walilipatia jeneza na kuelekea  msibani katika  mtaa wa uwanja wa Ndege kwa ajiri ya mazishi.
Baada ya kufika msibani hapo  taratibu za mazishi zilanza ambapo  waombolezaji walitangaziwa kuwa kabla ya mwili wa maremu  hauja pelekwa makaburini waombolezaji watauaga mwili wa Marehemu na wataanza kuaga wanaume kisha  wanawake .
Jeneza hilo lilifunguliwa  kwa ajiri ya  kuaga mwili wa marehemu ndipo waombolezaji walikuwepo msibani hapo waliposhikwa na mchangao  kuona jeneza likiwa tupu bila kuwemo ndani ya marehemu  ndani ya jeneza hilo .
Hari hiyo iliwafanya  ndugu wa marehemu waanze kuwahoji watu waliokuwa wamewagiza waufatie mwili wa marehemu kwenye chumba cha kuifadhi maiti kuwa mwili wa marehemu wameupeleka  wapi.
Kufatia majadiliano ya muda mrefu walifikia uamuzi wa kurudi kwenye chumba cha kuifadhi maiti katika hospitali ya Wilaya ya Mpanda na  waliweza kuukuta mwili huo ukiwa ndani ya chumba hicho na ndipo walipoupakia  kwenye gari na walipofika kwenye geti    la walinzi walizuiwa na walinzi kuutowa mwili huo kwa kile walinzi walichodai kuwa mwili wa marehemu walichauchukua na huo sio mwili wa ndugu yao.
Uongozi wa Hospitali uliingilia kati kutatua tatizo hilo la ndugu wa marehemu na walinzi kwa kuwaruhusu ndugu wa marehemu kuuchukuwa mwili wa marehemu na  mazishi yake yliweza kufanyika siku hiyo hiyo  majira ya saa moja  jioni

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Katavi yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa