Home » » WAWILI WAFUNGWA JELA MIAKA 40 KWA KUKAMATWA NA MENO YA TEMMBO

WAWILI WAFUNGWA JELA MIAKA 40 KWA KUKAMATWA NA MENO YA TEMMBO

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.

Na Walter Mguluchuma
Katavi
 Mahakama ya Wilaya ya Mpanda imewahukumu  watu wawili  Stephano   Jonas (22) na  Franko Hamisi( 18)  Wakazi  wa Makazi ya Wakimbizi ya Katumba Wilayani Mlele Mkoa wa Katavi wamehukumiwa jumla ya kifungo cha miaka 40 jela baada ya kupatikana  na hatia ya kukamatwa na meno ya  Tembo yenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 27
Hukumu hiyo ilitolewa hapo jana na Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Wilaya ya Mpanda Odira  Amwol baada ya Mahakama kulidhika na ushahidi uliotolewa  mbele yake  na upande wa mashitaka .
Awali katika kesi hiyo mwendesha mashitaka  mwanasheria wa Serikali  Jamila Mziray  alidai Mahakamani hapo kuwa watuhumiwa hao kwa pamoja walikamatwa hapo  mei 15 mwaka huu  majira ya saa tisa usiku wakiwa katika Kijiji cha Mnyaki Makazi ya Wakimbizi ya Katumba.
Mziray alieleza kuwa  watuhumiwa hao walikamatwa kufuatia  taarifa  walizokuwa wamezipata Askari wa  Hifadhi ya Taifa (TANAPA)  wa   mbuga ya Katavi na jeshi la Polisi Mkoa wa Katavi.
Alieleza baada ya kuwa wamepata taarifa hizo  Askari hao walikwenda kwenye Kijiji cha Mnyaki  na walifanikiwa  kuwakamata watuhumiwa  hao wakiwa na meno ya Tembo vipande  vitatu vyenye uzito wa  kilogramu  nane yenye thamani ya shilingi milioni 27,760,000 wakiwa wameyahifadhi chini ya kitanda katika  nyumba ya Jackisoni  Elasto ambae alikuwa ni mshitakiwa wa taatu.
Washitakiwa hao katika utetezi wao  walidai kuwa meno hayo ya Tembo hayakuwa yao bali yalikuwa  ni ya  Jackisoni  Elasto  ambae kwenye kesi hiyo alikuwa ni mshitakiwa wa tatu na alikuwa amewatuma wapeleke Daress  salaam kwa mtu mmoja anae julikana kwa jina la Alex na  wayasafirishe meno hayo kwa njia ya  Treni.
Hakimu  Amwol baada ya kusikiliza mwenendo mzima wa kesi hiyo na  ushahidi uliotolewa  mahakamani hapo  ambapo upande wa mashitaka ulikuwa  na  mashidi saba na washitakiwa walijitetea wenyewe  aliieleza Mahakama kuwa pasipo chaka yoyote  Mahakama imelidhika na ushahidi wa upande wa mashitaka  na watuhumiwa  wawili wamepatikana na hatia.
Hivyo  aliwapa nafasi watuhumiwa  ya kujitete kama watakuwa na sababu ya msingi ya kuishawishi mahakama iwapunguzie adhabu .
Mshitakiwa wa kwanza   Stephano  Jonas  aliiomba Mahakama impunguzie adhabu kwa kuwa mama yake mzazi na wadogo zake watatu wanamtegemea yeye .
Nae mshitakiwa wa pili  Franko Hamisi aliomba Mahakama impunguzie adhabu kwa kuwa  anaumri mdogo wa miaka 18 na mama yake mzazi anamtegemea yeye na pia hana baba kwani baba yake alishafariki Dunia.
Mwanasheria wa Serikali Jamila Mziray baada ya utetezi huo aliupinga vikali na aliiomba Mahakama itowa adhabu kulingana makosa  ya  vifungu vya sheria  walivyopatikananavyo  ili iwe fundisho pia kwa watu wengine  wenye tabia kama hizo.
Hakimu Odira Amwol baada ya kusikiliza ombi la washitakiwa  la kuomba kupunguziwa  adhabu  alisoma hukumu  kwa kueleza  kuwa  Mahakama  imewatia hatiani washitakiwa   Stephano Jonas  na Franko Hamisi na Mahakama imewakumu kutumikia  kila mmoja kifungo cha miaka 20 jela .
Mahakama hiyo ilimwachia huru mshitakiwa watatu Jackisoni Elasto baada ya kukosekana kwa ushadi   wa kumtia hatiani uliotolewa na upande wa  mashitaka .
Hivi karibuni Mahakama hiyo iliwahukumu watu wawili kutumikia jela  kifungo miaka 42 baada ya kupatikana na kosa la kukamatwa na meno ya Tembo ya thamani ya milioni 60.

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Katavi yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa