Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Na Walter
Mguluchuma
Katavi
Jeshi la Polisi
Mkoa wa Katavi
linawashikilia watu wawili
wakazi wa Tarafa ya Mpimbwe Wilaya ya Mlele Mkoani
hapa kwa tuhuma za kukamatwa
na meno ya Tembo manne yenye
uzito wa Kirogramu 47.6 yenye
thamani ya shilingi milioni 60 wakiwa wameyabeba kwenye Pikipiki
Watuhumiwa hao waliokamatwa walitajwa kuwa ni
Jastine Bruno (50) na Philiberti
Leo (Uliza) 35 Wakazi wa
Kata ya Usevya Tarafa ya Mpimbwe Wilaya ya Mlele
Kamanda wa Polisi
wa Mkoa wa Katavi Dhahiri
Kidavashari aliwaambia Waandishi wa
Habari jana kuwa
watuhumiwa hao walikamatwa
hapo juzi
majira ya saa moja na nusu
huko katika Kitongoji
cha Tompola Kata ya
Usevya
Alisema
kabla ya kukamatwa kwa Watuhumiwa hao
jeshi la Polisi na Askari
wa Hifadhi ya Taifa mbuga ya Katavi
walipata taarifa kutoka kwa Raia wema
kuwa watuhumiwa hao wamebeba meno ya
Tembo kwenye Pikipiki
Kamanda Kidavashari
alieleza kuwa baada ya kuwa taarifa
hizo zimefika kwa Askari wa Tanapa
Katavi na Jeshi la Polisi walishirikiana kuandaa mtego wa kuwakamata watuhumiwa hao wawili
Alisema ndipo walipoweza kufanikiwa kuwakamata
watuhumiwa hao wakiwa wamabeba meno hayo ya Tembo
kwenye Pikipiki yenye Namba za usajiri T 645 CUS
aina ya Toyo wakiwa wameyahifadhi kwenye
mfuko wa Salpheti
Baada ya kuwakamata
waliweza kuwepekua na ndipo walipo wakuta watumiwa wakiwa na meno hayo ya Tembo
manne wakiwa wameyahifadhi kwenye mfuko
Kamanda Kidavashari
alisema watuhumiwa hao wote
wawili wanashikiliwa na jeshi la Polisi kwa mahojiano zaidi na wanatarajiwa kufikishwa Mahakamani
upelelezi utakapo kuwa umekamilika
Pia amewataka
Wakazi wa Mkoa wa Katavi kuendelea na ushirikiano kwa jeshi la Polisi
kwa kuwafichua watu wanaojihusisha na vitendo viovu
0 comments:
Post a Comment