Home » » MTU NA MTOTO WAKE WAGOMBANIA UDIWANI KWA VYAMA TOFAUTI

MTU NA MTOTO WAKE WAGOMBANIA UDIWANI KWA VYAMA TOFAUTI

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 

Na  Walter  Mguluchuma
Katavi
 Uchaguzi  wa  Udiwani wa Kata ya  Magamba  Manispaa ya Mpanda Mkoa wa Katavi  ambao  ulishindwa kufanyika Oktoba  25  unatarajiwa kufanyika kesho huku ukiwa unawahusisha wagombea wawili  ambao ni mtu na mtoto wake
 Uchaguzi huo wa Udiwani wa Kata ya Magamba uliharishwa na tume ya uchaguzi kufuatia  kukosekana  kwa karatasi za kupigia kura za   nafasi ya  udiwani wa Kata hiyo
 Wagombea wa Udiwani wa Kata hiyo  wanatoka  kwenye vyama  vya   Demokrasia na  Maendeleo( CHADEMA)  na  Chama  cha Mapinduzi (CCM)
Ambapo   Chama cha Mapinduzi   kimemsimamisha   Philipo  Kalyalya Mpela  ambae  ni  baba wa  mgombea wa nafasi hiyo ya Udiwani  Joseph  Mpela  Kalyalya  (CHADEMA)
Kutokana na   nafasi  hiyo kugombewa na mtu na mtoto wake kupitia  vyama  tofauti  uchaguzi huo wa kesho umezuia  hisia  kubwa  za  wakazi  wa Manispaa ya  Mpanda  na Mkoa wa  Katavi kwa ujumla  wake
Kwa  upande  wake   Joseph  alisema   kuwa  yeye  aliamua kugombea  udiwani  baada  ya kuona  baba  yake  ameongoza kata hiyo kwa kipindi cha miaka  20  bila kuwaachia watu wengine  hivyo umefika wakati wa Kata hiyo kuongozwa nay eye ambae ni kijana
Nae  Katibu   Mwenezi wa CCM  wa  Mkoa wa Katavi   Joseph   Makumbule alisema  kuwa Chama  chake kimejipanga kuhakikisha wanashinda  kesho    kwani  katika  uchaguzi wa Oktoba  25  Chama  hicho kiliweza kuchinda  Kata  zote  14 za  Manispaa ya  Mpanda  hivyo wanataka kuendelea na rekodi hiyo
Katibu wa  CHADEMA  wa  Mkoa wa  Katavi  Alimasi  Ntije    alisema  wamejiandaa  kushinda  uchaguzi huo ili  waweze kuwa na  mwakilishi   mmoja  wa udiwani  ambae  atakuwa anaingia  kwenye  Baraza  la   Madiwani wa Manispaa ya Mpanda  anae  toka  kwenye  chama chao
Manispaa ya  Mpanda inajumla ya  Kata  15   ambapo  katika  uchaguzi  uliofanyika  hivi  karibuni   CCM walipata  ushindi  katika  Kata  hizo  zote

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Katavi yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa