Home » » HATARI: AKUTWA AKIWA AMEUWAWA NA KUNYOFOLEWA SEHEMU ZAKE ZA SIRI NA VIDOLE 4 NA KUNYOLEWA NYWELE KICHWANI

HATARI: AKUTWA AKIWA AMEUWAWA NA KUNYOFOLEWA SEHEMU ZAKE ZA SIRI NA VIDOLE 4 NA KUNYOLEWA NYWELE KICHWANI

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 

Na  Walter  Mguluchuma 
Katavi
Mtu  mmoja  aliyefahamika  kwa  Jina  la   Chiza  Lameck (23)  Mkazi wa Kijiji  cha  Mgansa Wilaya ya Mpanda Mkoani  hapa  amekutwa akiwa  ameuwawa  na mwili  wake  kutelekezwa  shambani  katika kijiji cha jirani  huku mwili wake ukiwa umenyofolewa  sehemu zake za siri, vidole vinne  vya mkono na  kunyolewa nywele upande mmoja wa kichwa chake
Kamanda wa  Polisi wa  Mkoa wa  Katavi  Dhahiri  Kidavashari aliwaambia  Waandishi wa  Habari kuwa  tukio  la mauwaji  hayo  lilitokea  hapo  Novemba   sita  katika  Kijiji  cha Ilangu
 Alisema  kabla ya tukio  hilo   kutokea   marehemu  katika uhai  wake  alikuwa akisumbuliwa  na tatizo  la ugonjwa wa  akili
  Alieleza  kuwa  marehemu alitoweka nyumbani kwake   kuanzia  tarehe  2  Novemba  na  ndugu  zake walimtafuta  bila  mafanikio  yoyote
 Kidavashari  alisema  ndugu wa Marehemu walipata taarifa Novemba 6  kuwa  mwili wa marehemu  Chiza umeonekana ukiwa katika Kijiji cha jirani cha Ilangu  ukiwa umetelekezwa kwenye  shamba
Baada ya kuwa wamepata taarifa  hizo  ndugu  wa  marehemu  walifika  kwenye  eneo  hilo na  walikuta  mwili wa  ndugu yao ukiwa umetelezwa  shambani
 Alisema  baada ya kuufanyia  uchunguzi  wa  awali  walikuta  mwili wa marehemu ukiwa  na  mapungufu  kadhaa kwani  sehemu za siri  za mwili wake   zilikuwa  zimenyofolewa , vidole  vyake vinne  vya mkono wa kushoto na   kunyolewa  nywele sehemu  moja ya upande wa kichwa  chake
 Alieleza  uchunguzi wa  awali  onaonyesha kuwa  chanzo  cha mauwaji  hayo  kilisababishwa  na imani za ushirikina 
 Kidavashari  alieleza  kuwa  mpaka sasa  hakuna  mtu wala  watu  aliyekamatwa  kuhusiana  na  tukio la mauwaji  hayo  na jeshi  la Polisi  kwa kushirikiana  na Wananchi wanaendelea  na msako wa kuwabaini  waliohusika  na mauwaji  hayo

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Katavi yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa