Home » » HOT: MWANAFUNZI ALIYETAKA KUOZESHWA NA WAZAZI WAKE KWA NGUVU AFANYA MTIHANI WA TAIFA WA DARASA LA NNE

HOT: MWANAFUNZI ALIYETAKA KUOZESHWA NA WAZAZI WAKE KWA NGUVU AFANYA MTIHANI WA TAIFA WA DARASA LA NNE

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Na  Walter  Mguluchuma
Katavi
Mwanafunzi wa  Darasa la  nne  wa  Shule ya Msingi  Mwamkulu Manispaa ya  Mpanda  Mkoa wa  Katavi  Manisiter   Joe (14) ambae wazazi wake  walitaka kumwozesha kwa nguvu na ndoa yake kuvunjika kabla haija fungwa amefanya mtihani wa Taifa  wa Darasa la  nne chini ya usimamizi wa ofisi ya  maendeleo na ustawi wa Jamii ya Manispaa ya Mpanda
Mwanafunzi huyo  alikuwa  ameachishwa na   masomo  na  wazazi wake   na kuamua  kumwozesha kwa aliyewahi kuwa  mwanafunzi  mwenzake wa shule  hiyo baada ya wazazi wake kuwa  wamepokea  mahari ya  Ng’ombe 15
 Hivi  karibuni  ofisi ya  Elimu  ya  Manispaa ya  Mpanda  kwa kushilikiana  na  jeshi  la  Polisi  Mkoa wa  Katavi walifanikiwa   kusitisha  ndoa ya  mwanafunzi huyo aliyetaka  kuozeshwa   kwa nguvu ya wazazi  pasipo kuwa na ridhaa yake mwenyewe muda mfupi kabla ya ndoa yake  kimila  kufungwa katika  Kijiji  cha  Mwamkulu  Wilayani   hapa na kijana huyo huku  akiwa amevarishwa  shela  tayari  tayari kwa ndoa kufungwa  kwa ndoa hiyo ilivutia hisia  za watu wengi wa Mkoa wa Katavi na nje ya Mkoa
Akizungumza  na Waandishi wa Habari  hapo  jana  Ofisini  kwake  Afisa  Elimu wa Manispaa ya Mpanda Vicent Kayombo  alisema kuwa  Mwanafunzi  huyo  baada ya kuwa  ametendewa hivyo  na baba yake  mzazi  Manispaa ya  Mpanda iliamua kuchukua jukumu la kumuumishia  yule ya Msingi Azimio ambayo ipo  katikati ya Manispaa ya Mpanda huku akiwa chini ya uangalizi  wa  idara ya  maendeleo na ustawi wa  jamii
Kayombo  alifafanua kuwa   pamoja na kuwamwamishia  kwenye  shule  hiyo  amelazimika  kwenda  kufanya  mtihani wa Taifa wa  Darasa  na nne kwenye  shule yake ya  zamani ya Mwamkulu kwa kuwa alikuwa amesajiriwa kufanyia  mtihani  kwenye  shule hiyo
 Alisema  ameondoka  leo  yaani  jana kwenda kufanya mtihani huo  huku  akiwa  amesindikizwa na  Afisa  Maendeleo   wa  Ustawi wa Jamii wa Manispaa ya  Mpanda  ambae akuwa  nae huko  hadi atakapo kuwa  amemaliza  mitihani yake na kisha  atarudi  nae  mjini  Mpanda
 Alieleza   baada ya  kumaliza  mitihani  hiyo  ataendelea  na  masomo   kwenye  shule ya Msingi  Azimio  na sio   Mwamkulu  tena  kwani  Manispaa ya Mpanda  imeisha  chukua jukumu la kumuhamisha  kwenye  shule yake za  zamani
 Alisema  pamoja  na  baba  mzazi wa mtoto huyo  ambae  alitoroka   baada ya  jaribio  lake  la kutaka kumwozesha  kushindikana  mwanafunzi  huyo  ameonyesha  nia  ya  kuendelea  na  masomo  na  amemwakikishia  Afisa  Elimu wa Manispaa kuwa  lazima  atafaulu  mtihani wa Taifa wa Darasa  la  nne  na ule wa kumaliza  darasa   la  saba
Pamoja  na juhudi   hizo za kumnusuru  mwanafunzi huyo   baba  mkubwa wa  mtoto huyo   nae  pia    ameonyesha nia za kutaka  kumchukua  mtoto huyo ili aweze  kuendelea   na  masomo  katika  shule  hiyo ya Azimio  na  amepinga  vikali  kitendo hicho  cha mdogo wake  alisema  Kayombo
 Alisema   wanaangalia  namna ya  kuweka  utaratibu  wa  kumkabidhi  baba yake mkubwa  na  mtoto huyo ila kwa masharti ya kuhakikisha  mwanafunzi huyo  anaendelea na masomo yake  kama  kawaida
Manispaa ya Mpanda kwa kipindi cha miaka miwili mfululizo sasa ndio inayoongoza  kwa matokeo ya ufaulu wa wanafunzi wa Darasa la saba Kitaifa

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Katavi yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa