Home » » WATU WAWILI WAFA BAADA YA KUGONGWA NA GARI

WATU WAWILI WAFA BAADA YA KUGONGWA NA GARI

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 

Na  Walter Mguluchuma
Katavi
Watu wawili   Mshaki  Mashauri(22) na Victoria  Mbas(28) wakazi wa Kijiji cha Usevya Wilaya ya Mlele Mkoa wa Katavi wamefariki Dunia  baada ya kugongwa na gari  wakati wakiwa wamepakizana kwenye baiskeli
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Katavi Dhahiri Kidavashari aliwaambia Waandishi wa Habari  jana kuwa tukio  hilo lilitokea  hapo jana  katika  eneo la Kagera Kata ya Kibaoni  Wilaya ya Mlele  majira ya saa kumi na moja jioni
Kamanda Kidavashari alisema  ajari hiyo ya  gari  ililihusisha gari  No 504 CFA  aina ya Toyota Rav4 iliyokuwa ikiendeshwa na Dreva  Zakaria Feliki(47) Mkazi wa Kata ya Usevya Wilaya ya Mlele
 Alisema gari hilo  lilikuwa  lilikuwa likitokea  katika Kijiji cha Kibaoni likiwa linaelekea  katika  Kijiji cha  Usevya  Tarafa ya Mpimbwe
 Gari hilo lilipofika  maeneo ya Kagera  Kata ya Kibaoni  lilimgonga mwendesha  baiskeli  Mtaki  Mashauri  na abilia wake   Victoria Mbas na kuwasababishia vifo  ambapo  Mtaki alifariki hapo hapo kwenye  eneo la tukio na Victoria alifariki Dunia muda mfupi baada ya kuwa amefikishwa  Zahanati ya Kibaoni
 Alisema  Dreva wa gari lilo  alikamatwa  na  anashikiliwa na jeshi la polisi  na gari lake  limehifadhiwa katika kituo cha polisi cha kibaoni wakati uchunguzi ukiwa  bado unaendelea
Kindavashari alieleza  kuwa  mili ya marehemu wote  wawili  imehifadhiwa  katika  chumba cha kuhifadhi  maiti  katika hospitali ya Wilaya ya Mpanda  kwa ajiri ya uchunguzi
Chanzo cha  ajari hiyo ilitokana  na mwendo kasi wa gari ambapo dreva wa gari hiyo alikuwa akishindani  kukimbia mwendo kasi na mwendesha pikipiki
Mtuhumiwa anatarajiwa kufikishwa mahakamani  mara baada ya uchunguzi utakapo kuwa umekamilika  ili aweze kujibu mashitaka yanayomkabili

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Katavi yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa