Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Na Walter Mguluchuma
Katavi
Watu watano wamekufa hapo hapo na wengine watano kujeruhiwa Wilayani Mlele Mkoa wa Katavi baada ya gari walilokuwa wakisafiria aina ya Noar kupinduka
Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Katavi Dhahiri Kidavashari ajari hiyo ilitokea jana majira ya saa tisa alasiri katika eneo la Kijiji cha Matandalani Wilayani Mlele
Alisema ajari hiyo ililihususha gari lenye Namba za usajiri T451 DDP lililokuwa likiendeshwa na Dreva Justine Ndayele (24) mkazi wa Mkoa wa Kigoma gari hilo mali ya Adamu Omary lilikuwa likitokea Mjini Mpanda kuelekea katika Kjiji cha Sitalike Wilayani Mlele
Kamanda Kidavashari aliwaja waliokufa kwenye ajari hiyo kuwa ni Lunyalaja Nzugamrwa(50) 2Furaha Eduard (35)Eva Mwanisawa (25) Maiko Jacob wakazi wa Kijiji cha Sitalike na Mwila Kifwewe(25) Mkazi wa Mtaa wa Kawajense mjini Mpanda
Alisema mili ya marehemu hao wote watano imehifadhiwa katika chumba cha kuhifadhi maiti katika hospitali ya Wilaya ya Mpanda
Kamanda Kidavshari aliwataja majeruhi wa ajari hiyo kuwa ni Felista Matunda (30) mkazi wa Tarafa ya Inyonga Thobias Kisila (65)mkazi wa Kijiji cha Sitalike Velina Libaratu (9) mkazi wa Tarafa ya Mpimbwe Odila Lenatusi (19)Ndila Kameme (32)wakazi wa mtaa wa Nsemlwa mjini Mpanda
Alisema majeruhi hao wamelazwa katika hospitali ya Wilaya ya Mpanda wakiwa wanaendelea kupatiwa matibabu huku hari zao zikiwa zinaendelea vizuri
Kidavashari alieleza kuwa ajari hiyo ilisababishwa na mwendo kasi wa gari hari ambayo ilisababisha gari kuacha njia na kupinduka na kusabisha vifo vya watu hao watano kufa hapo hapo
Polisi wanamshikilia dreva wa gari hilo na upelelezi wa tukio hilo utakapo kamilika wanatarajia kumfikisha mahakamani ili akajibu mashitaka

0 comments:
Post a Comment