Home » » WAANDISHI WA HABARI WATAKIWA KUFAHAMU VEMA WAJIBU WAO

WAANDISHI WA HABARI WATAKIWA KUFAHAMU VEMA WAJIBU WAO

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 

Na  Walter  Mguluchuma
Katavi
Waandishi wa habari  wametakiwa  wafahamu  vyema wajibu  misingi  na mipaka  ya majukumu  yao ya  kiutendaji  na kitaaluma  kwa kila siku
Hayo yalisemwa  hapo jana na  Katibu  Tawala wa Mkoa wa Katavi Mwandisi  Emanuel Kalobelo  wakati akifungua mkutano wa wadau wa  habari wa Mkoa wa Katavi katika  mkutano uliofanyika  katika ukumbi wa mtakatifu Maria mjini Mpanda mkutano huo uliandaliwa na Chama cha Waandishi wa habari cha Mkoa wa Katavi(KPC)
Alisema  waandishi wa habari  wanahitajika   kubeba  dhamana ya uwajibikaji bora  tena uliotukuka  kwa kutenda  haki  na kuwa  wazi  sana  katika shughuli zao  za kila siku  za kupasha habari  na kuelimisha jamii na katika nyakati za uchaguzi
Mwandisi  Kalobelo  alieleza vyombo  vya habari  vinatakiwa kuwa  huru  na  kutekeleza majukumu  yake  bila upendeleo   na kukandamiza  ama kuumiza upande  mwingine  na huo ndio msingi  wa maadili  ya kazi  za wanaabari
Alifafanua  kwamba  kutokana  na unyeti  wa  shughuli  za uchaguzi  kipindi cha uchaguzi  waandishi wa  habari  wanatakiwa kuongeza  umakini  maradufu katika utendaji  wao wa kazi  ili kuisaidia jamii na Taifa  kwa ujumla  kuchunga  na kulinda  na kuhifadhi  amani  ya nchi  isitetereke
 Alisema waandishi wa habari  wanapoandika habari za upande mmoja   na kupendelea  kwa kukandamiza upande mwingine  wanakuwa hawatoi  nafasi  kwa upande wa pili  kwa kutosiliza   maoni   yao  jambo hilo ni baya  na  ni kiashiria  tosha  cha uvunjifu wa amani
Wananchi  wanavipenda  na  kuviamini  sana  vyombo vya habari pale  vinapojitahidi  kufanya kazi zao  kwa umakini ,uwazi  na tena  bila  kuegemea  upande wowote alisema  Mwandisi Kalobelo
Hivyo  vyombo vya habari  vinatakiwa  vibebe  pia wajibu  wa kuunganisha jamii na sio kuifarakanisha  kwa sababu ya  kutumiwa na  vyombo  vyama vya siasa  ama watu binafsi  kwa  maslahi yao
Kwa upande wake afisa wa kutoka  TAKUKURU  Mkoani  Katavi  Simon  Buchwa  alisema kuwa  waandishi wa habari wanawajibu wa kufanya kazi kwa  kuzingatia maadili yao
Alisema wapo baadhi ya waandishi wa habari wamekuwa wakipokea rushwa ili kuwaandika  kuwachafua watu na wengine  kuwaandika vizuri hilo ni kosa

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Katavi yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa