Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Na Walter
Mguluchuma
Katavi
Mgombea Ubunge wa
Jimbo la Mpanda Mjini (CHADEMA) Jonas
Kalinde amekamatwa akiwa na wafuasi kumi wa chama hicho kwa tuhuma za
kufanya maandamano bila kibali
Kalinde na wafuasi hao walikamatwa hapo
jana majira ya saa kumi na mbili na
nusu jioni katika eneo la
mtaa wa Majengo A Mjini hapa
Mgombea huyo
alikamatwa wakati akiwa anatokea kwenye mkutano wa kampeni za ubunge
wa jimbo la Mpanda mjini
uliofanyika katika mtaa wa
Kigamboni Kata ya Shanwe
Wanadaiwa mara
baada ya kumalizika kwa mkutano wa kampeni mgombea huyo na wafuasi wa Chama
hiyo walianza kutembea kwa miguu kwa lengo la kwenda
kwenye ofisi za Chadema zilizoko
katika mtaa wa Majengo
Wakati wakiwa njia walipofika
eneo la Posta walikamatwa na polisi
na walipelekwa kituo cha
polisi cha Mpanda mjini kwa ajiri ya mahojiano
Kwa upande wake
Jonas Kalinde alisema kuwa alilazimika
kutembea kwa miguu yeye na wafuasi wake
mara baada ya kumalizika kwa mkutano kutokana na gari anayoitumia
kulete hitilafu
A lisema
baada ya kukamatwa walifikishwa
kituo cha polisi ambako walikaa mpaka
saa tatu na nusu ndipo waliweza kupatiwa
mdhamana na kuambiwa kesho arudi tena
Kamanda wa Polisi
wa Mkoa wa Katavi Dhahiri
Kidavashari alithibitisha kukamatwa kwa mgombea ubunge huyo
Pia amewataka
viongozi wa vyama vya siasa kufuata
sheria na taratibu zilizowekwa na tume ya uchaguzi
0 comments:
Post a Comment