Home » » HOT NEWS :MWANAMKE AKAMATWA AKIWA ANAORODHESHA MAJINA NA VIPALATA VYA KUPIGIA KURA‏

HOT NEWS :MWANAMKE AKAMATWA AKIWA ANAORODHESHA MAJINA NA VIPALATA VYA KUPIGIA KURA‏

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 
Na  Walter  Mguluchuma
Katavi
Jeshi la Polisi  Mkoa wa Katavi linamshikilia Salome Makala(32) Mkazi wa Kijiji cha  Mwenge  Kata ya Nsimbo Wilaya ya Mlele Mkoani  hapa kwa tuhuma ya kuwaorodhesha majina  wanakijiji wenzake  na  namba za  vipalata vya kupigia kura
Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Katavi Dhahiri Kidavashari mtuhumiwa alikamatwa hapo juzi majira ya saa nne usiku  katika Kijiji  hicho cha Mwenge
 Alisema mtuhumiwa huyo alikamatwa kufuatia taarifa zilizotolewa kwa jeshi la Polisi  kutoka kwa mgombea  ubunge wa Jimbo la Nsimbo  Gerald Kitabu(CHADEMA)
Alisema  baada ya polisi kupata taarifa hizo  walifika kwenye  kijiji hicho na kumkuta  salome akiwa na orodha ya  majina ya wanakijiji wenzake na namba za vipalata vya kupigia kura akiwa  ameandika kwenye daftari lake
Kidavashari alisema Polisi walimkamata mtuhumiwa na kumfikisha kwenye kituo cha polisi  cha Nsimbo kwa ajiri ya mahojiano
 Alieleza  baada ya mahojiano  mtuhumiwa   alieleza  kuwa  alikuwa anakusanya  taarifa  za  Wanachama  wa umoja wa wanawake wa CCM(CWT) kwa kuwa katika kijiji hicho cha Songambele  akikuwa na kumbukumbu zozote
 Kidavashari   alisema Jeshi la Polisi  bado linaendelea  kumhoji mtuhumiwa Salome Makala  ili kuweza kupa ukweli zaidi wa tukio hilo

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Katavi yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa