Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Na Walter Mguluchuma
Katavi
Mgombea Ubunge wa
vyama vinavyounda umoja wa
Ukawa(CHADEMA) wa Jimbo la
Mpanda vijijini Mussa
Masanja Kantambi amepata
kipigo na gari yake kushambuliwa kwa mawe na kujunjwa kioo cha mbele baada
ya kupita kwenye eneo walilokuwa wakifanyia mkutano wa kampeni za Mgombea
Ubunge wa CCM
Tukio la kupingwa kwa mgombea huyo lilitokea hapo
juzi majira ya saa sita
mchana katika eneo la
Santamaria Katika Mtaa wa Mwamkulu Manispaa ya
Mpanda Mkoa wa Katavi
Siku hiyo ya
tukio Massanja alikuwa
akitokea mjini Mpanda
akiwa na gari
lake aina ya Land Cruiser
yenye namba za usajiri T390 ANM
huku akiwa anaelekea
kwenye kijiji cha
Kabage kwa lengo la kwenda kufanya mkutano wa kampeni ya kugombea Ubunge wa
Jimbo la Mpanda vijijini
Wakati akiwa
amefika kwenye eneo
hilo la Santamaria
alikuta mgombea Ubunge wa
Jimbo la Mpanda Mjini
Sebastiani Kapufi(CCM) akiwa anafanya
mkutano wake wa kampeni za ubunge
wa jimbo la Mpanda Mjini
Mgombea huyo wa
Ukawa baada ya kuwa amefika kwenye eneo hilo la mkutano wa mgombea wa CCM alisimamisha gari
lake karibu na eneo hilo la mkutano kwa kile alichodai
kuwa ameshindwa kuendelea na safari yake
kwa vile barabara ambayo alitaka
kupita imefungwa na watu waliokuwa kwenye mkutano huu
Kitendo hicho cha kusimamisha gari
karibu na mkutano huo kiliwakasilisha wafuasi wa CCM na kuamua kutoka kwenye
mkutano na kwenda kumvamia
mgombea huyo wa Ukawa na kuanza kumpa kipigo
Baada ya
kuona kichapo kimezidi mgombea
huyo alitimua mbio na kwenda kujihifadhi kwenye
nyumba moja iliyokuwa jirani huku
baadhi ya wafuasi wa CCM wakiwa wanalishambulia gari lake kwa mawe na kulivunja
kioo cha mbele
Kamanda wa Polisi
wa Mkoa wa Katavi Dhahiri Kidavashari
amekiri kutokea kwa tukio hilo
hapo juzi katika eneo la
Santamaria Mtaa wa Mwamkulu
Alisema tukio hilo lilitokea ila
viongozi wa vyama hivyo
waliamua kumaliza tatizo hilo wao wenyewe kwa kufanya
mazungumzo baina yao
Pia alisema jeshi la Polisi Mkoa wa Katavi limeandaa mkutano hapo
septemba 25 unakao wahusisha viongozi wa
madhehebu yote ya dini , viongozi wa vyama vya siasa na wazee mashuhuri
ili kujadiliana na mmna ya kudumisha
amani katika kipindi hiki cha uchaguzi
0 comments:
Post a Comment