Home » » MGOMBEA UBUNGE AITAKA WIZARA YA ELIMU KUFUNDISHA SOMO LA UZAZI WA MPANGO MASHULENI

MGOMBEA UBUNGE AITAKA WIZARA YA ELIMU KUFUNDISHA SOMO LA UZAZI WA MPANGO MASHULENI


Na  Walter  Mguluchuma
Katavi
Mgombea Ubunge wa Jimbo la Mpanda  Mjini (CHADEMA)   Jonas Kalinde  ameitaka   Wizara ya Elimu  iboreshe mitaala  yake  kwa   kuanza kufundisha   somo la elimu  ya  uzazi wa mpango  mashuleni  na  kwenye vyuo mbalimbali
Kauli hiyo aliitowa hapo jana  mbele ya waandishi wa habari  katika   Ukumbi wa White Club  Mjini  Mpanda
Kalinde alisema  Wanawake wengi   hawana elimu    ya kutosha ya uzazi wa mpango  suala ambalo linasababisha   mimba  na  zisizotarajiwa na  vifo  kutokana na Wanawake kutofahamu  toka mapema uzazi wa mpango
 Alisema huduma   huduma  za  uzazi wa Mpango  na huduma za afya  kwa akina mama  na watoto  wachanga  ni  muhimu  sana zikatolewa  bure nchi nzima  kuanzia Mijini , Vijijini na  hata kwenye  taasisi  za elimu  ili  kuweza kupunguza  vifo  vya  akina  mama  wajawazito   na watoto wachanga
 Alifafanua kuwa Serikali  haina budi  kulipatia  kipaumbele  suala la uzazi wa mpango  ili  kuwawezesha  akina  mama  wote kufikiwa  na huduma  hizi   nchi  nzima
Hivyo  alisema kuwa  endapo  atachaguliwa kuwa Mbunge  atahakikisha  elimu  ya uzazi wa mpango  inatolewa  mashuleni  na  vyuoni  kwa kutowa semina  na kusambaza  vipeperushi
 Pia  atapigania   ongezeko la  bajeti  ya Wizara  ya afya   hususani  katika uboreshaji  wa huduma   wa  huduma   za  uzazi  wa mpango  pamoja  na huduma ya  mama na mtoto mchanga
Vilevile   atashirikiana na wadau  mbalimbali  pamoja na  AZAKI  kuishawishi Serikali  kuongeza bajeti  kwenye ngazi ya  Serikali kuu  na   kwenye  Halmashauri
Nae Galus  Mgawe  Mgombea  Ubunge wa Jimbo hilo la  Mpanda Mjini  kupitia ACT  Wazalendo alieleza kuwa  wanawake wengi  na watoto wachanga  hupoteza  maisha  wakati wa  kujifungua  kutokana na kukosa  huduma   sahihi za afya  kabla  na  baada ya kujifungua
 Alisema  endapo atachaguliwa kuwa Mbunge  atatumia sehemu ya mshahara wake  wa ubunge  pamoja  na misaada ya wafadhili  katika kuboresha  huduma za uzazi wa mpango  na huduma  za   mama na mtot o mchanga
 Alieleza  kuwa atawasaidia   wanafunzi  wanaotoka  kwenye  familia   duni  misaada  mbalimbali ili  kupunguza  idadi  ya wasichana  wanaoacha   masomo  kwa  kukosa uwezo   fedha   hili  kupunguza  tatizo  la mimba za utotoni
Alisema  kitu cha msingi kwa yeye  ni kuwa  na takwimu  sahihi  za hali  ya huduma  za elimu  ya uzazi  wa  na elimu  za  afya ya   mama na mtoto  za kila eneo la nchi na jimbo lake na kuishawishi Wizara  na Halmashauri  kuongeza bajeti  itakayotokana na mapungufu  yatakayokuwa  yanajioonyesha kwenye  takwimu

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Katavi yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa