Home » » MWANAKIJIJI AUWAWA KIKATILI AKIWA AMELALA NYUMBANI KWAKE

MWANAKIJIJI AUWAWA KIKATILI AKIWA AMELALA NYUMBANI KWAKE

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 

Na  Walter Mguluchuma
Katavi
Mtu  mmoja mkazi wa Kijiji  cha  Ikingwamiza  Kata ya Mwamapuli  Tarafa ya Mamba Wilaya ya Mlele Mkoa wa Katavi ameuwawa  kikatili kwa kukatwa katwa na mapanga  na watu wasiojulikana wakati akiwa amelala nyumbani kwake usiku
 Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Katavi Dhahiri Kidavashari  alimtaja  mtu huyo aliyeuwawa kikatili kuwa ni   Shija  Nkingo (60)  Mkazi wa Kijiji cha  Ikingamiza Tarafa ya Mamba Wilaya ya Mlele
Kidavashari aliwaambia Wahandishi wa Habari kuwa tukio hilo la mauwaji ya kikatili lilitokea  Septemba 10   mwaka huu majira ya saa saba usiku nyumbani kwake na marehemu Shija  Nkingo
 Alisema wauwaji hao ambao hawajafahamika siku hiyo ya tukio walifika nyumbani kwa marehemu  majira ya saa saba usiku uku  wakiwa na mapanga   na marungu
 Alieleza baada ya kufika nyumbani kwa marehemu wauwaji hao  walivunja mlango wa nyumba ya marehemu  na kisha waliingia ndani ya nyumba yake 
Baada ya kuwa wameingia ndani  walimkuta marehemu akiwa amelala na kisha walianza kumshambulia kwa kumkata kata kwa mapanga sehemu mbalimbali za mwili  wake  mpaka kupelekea mauti yake
 Kamanda Kidavashari alisema baada ya kufanya mauwaji hayo ya kikatili wauwaji hau walitokomea  mahari kusiko julikana  na majirani walifika kwenye eneo hilo na kukuta mwili wa marehemu ukiwa chini ya kitanda huku ukiwa umekatwa katwa vibaya kwenye sehemu mbali mbali za mwili wake
 Alisema chanzo cha mauwaji hayo bado haki fahamika  mpaka sasa na  hakuna watu waliokamatwa kuhusiana na mauwaji hayo
Kamanda Kidavashari  alieleza kuwa  Jeshi la Polisi kwa kushirikiana na  uongozi wa Kijiji cha Ikingwamiza  wanaendelea  na uchunguzi  ili kuwabaini watu waliohusika  ili waweze kuwakamata  na kuwafikisha kwenye vyombo vya sheria

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Katavi yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa