Home » » HOT NEWS: MBUNGE WA CHADEMA AJIUNGA NA ACT WAZALENDO

HOT NEWS: MBUNGE WA CHADEMA AJIUNGA NA ACT WAZALENDO

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 


Na  Walter  Mguluchuma 
Katavi
 Mbunge wa viti maalumu(CHADEMA)  Anastella  Malack  ambae  amemaliza muda wake  jana  ametangaza rasmi  kujiondoa  CHADEMA  na kurudisha  kadi ya  chama hicho  na  kujiunga na  chama cha ACT Wazelendo na kukabidhiwa kadi ya  chama cha ACT   Wazalendo
Malack  alirudisha kadi hiyo hapo jana kwa kiongozi mkuu wa  chama cha ACT wazelendo  Zitto  Kabwe kwenye mkutano wa hadhara uluofanyika  katika  uwanja wa Kashaulili  Mjini  hapa
Katika  mkutano  pia  aliyekuwa diwani wa Kata ya  Makanyagio  (CHADEMA) I ddy  Nzyiguye  alitangaza  rasmi kujiunga  na  chama  cha   ACT   baada ya kurudisha  kadi ya  CHADEMA na kukabidhiwa kadi ya  ACT  wazelendo
Kabla ya kuwakabidhi kadi za  Chama  hicho   Zitto  Kabwe alipokea  kadi za kutoka  kwenye  vyama  mbalimbali ambazo wanachama wa vyama hivyo walimkabidhi na kasha  aliwapatia  kuwapatia  kadi za  ACT wazalendo
Katika  hotuba  yake ya kuwapokea  walokuwa wanachama  hao na viongozi kupitia  chama hicho  aliwataka  viongozi  wa ACT  kutozitupa  kadi hizo  zilizo rudishwa wala kuzichoma moto na badala yake   wazirudishe kwa makatibu wa  Mikoa husika  ambako wanachama hao waliko toka
Pia  aliwataka wanchi wa Mkoa wa Katavi kuwachagua viongozi  ambao  wanania ya kuleta maendeleo kwa wananchi wao
 Alisema wapo baadhi ya watu wnataka wachaguliwe  kwa manufaa yao binafsi badala ya manufaa ya wananchi waliowachagua
Vilele  aliwaambia  Wananchi hao kuwa   chama  chake cha ACT  wazalendo kitaweka wagombea wa nafasi za ubunge katika majimbo yote matano ya Mkoa wa Katavi na wagombea Udiwani  katika  kata zote  54 za Mkoa wa Katavi
Kwa upande  wake aliyekuwa  mbunge wa Viti  Maalumu    Annastela  Malack  aliwataka wananchi wa Mkoa wa Katavi kushikamaene ili  kuleta maendeleo  katika Mkoa huo
Alisema  Mikoa ya  Katavi  Tabora  , Kigoma  na Rukwa  ipo  nyumba kimaendeleo  hivyo  bila kuwepo na  mshikamano  ya wananchi wanao ishi kwenye mikoa hiyo maendeleo hayatakuwepo

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Katavi yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa