Home » » MAJAMBAZI WAVAMIA KIJIJI WAKIWA NA SILAHA 2 ZA KIVITA NA KUPOLA ZAIDI YA MILIONI SABA NA SIMU

MAJAMBAZI WAVAMIA KIJIJI WAKIWA NA SILAHA 2 ZA KIVITA NA KUPOLA ZAIDI YA MILIONI SABA NA SIMU

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 

Na  Walter Mguluchuma 
Katavi
Watu wanne  wanaosadikiwa kuwa ni  majambazi  wakiwa na silaha  mbili za kivita  aina ya  SMG  wamewavamia wafanya biashara wa kununua  mpunga  katika  Kijiji  cha  Vikonge Wilaya ya Mpanda  Mkoa wa Katavi na kupola  kiasi cha zaidi ya shilingi  milioni  saba  na simu
Kamanda wa polisi wa Mkoa wa Katavi Dhahiri Kidavashari  aliwaambia Wahandishi wa  habari  kuwa tukio  hilo la upolaji lilitokea  hapo   Agosti 16 majira ya saa saba usiku
 Kidavashari  alisema   siku  hiyo ya tukio majambazi  hao  wakiwa  na silaha  mbili  za kivita  aina  ya SMG  waliwavamia Wafanyabiashara  na kufanya  upolaji  wa fedha kiasi cha  Tsh 7,180,000  na simu mbili zenye  thamani ya Tsh 5,000,000
  Katika  tukio hilo  Majambazi hao waliwapola  Siasa  Simon( Kasumuni )   mkazi  wa Kasulu  Kigoma   aliyepolwa kiasi cha  Tsh 5,000,000 simu moja aina ya Techno yenye   thamani ya shilingi  laki  mbili na nusu  na kadi ya  Benki ya CRDB
Kidavashari alimtaja  mfanyabiashara  mwingine  aliyepolwa kuwa ni Edward Filemon(Mnonga) Mkazi wa Kasulu Kigoma  alipolwa  Tsh 2,180,000 simu  moja aina ya  Techno yenye  thamani ya Tsh 250,000 pia  alijeruhiwa  baada ya kupigwa  malungu   katika  mkono wake wa kushoto na  kumsababishia  maumivu  makali
 Kabla ya  tukio   hilo wafanyabiashara hao wawili  walikuwa wamefika kijijini  hapo  mnamo tarehe  15 Agosti  kwa lengo la kununua  mpunga  kutoka kwa wakulima wa Kijiji  hicho
 Alisema  siku  hiyo  wakati wakiwa wamelala  katika  nyumba  waliokuwa wamefikia Kijijini  hapo   ya Mnyaga  Maziku  ndipo  majambazi   hao  walipowavamia   kwa   kuvunja  mlango  na kisha waliingia  ndani na kufyatua risasi  sita  na kisha  walifanya uporaji  huo
 Jeshi la Polisi  kupitia kwa raia wema  walipata taarifa  na kuwahi  katika eneo hilo  na baada ya kufika walishirikiana na Sungsungu  wa eneo hilo  ambapo walifuatilia  nyayo za majambazi hao  hadi kwenye pori la  Luhafe na walifanikiwa kuwaona majambazi hao wakiwa umbali wa mita 150 na kisha walianza kuwakimbiza
Alisema majambazi hao baada ya kuona karibu wakamatwe waliamua kutupa  chini  mfuko wa  salphate na kutokomea  porini kusiko julikana
Baada ya upekuzi  kufanyika  kwenye mfuko huo  kulikutwa  na  silaha  mbili  za kivita  aina ya SMG  zenye  Namba UA-3379  na 19111685 ikiwa na risasi 23 pia katika eneo hilo la tukio  yaliweza kupatikana  maganda matatu  ya risasi  za bunduki  aina ya SAR  na  SMG
Kamanda Kidavashari aliwaeleza waandishi wa Habari kuwa   jeshi la Polisi  limefanikiwa  kuwakamata watuhumiwa wanne  ambao bado wanaendelea kushikiwa na jeshi  la  Polisi
 Aliwataja watuhumiwa hao walikamatwa kuwa ni Mayunga   Saguda (44) Halila  Tiga(33) Mnyaga  Maziku(30) wakazi wa  Kijiji cha Luhafe Wilaya ya Mpanda na  Shija  Mahoma (30)  Mkazi wa  Mtaa wa Kawajense  Mjini  Mpanda
Kamanda wa Polisi wa  Mkoa wa Katavi  ameendelea  kuwashukuru Wananchi  wanaoendelea  kushirikiana  na jeshi la Polisi  katika kufanikisha kudhibiti  vitendo vya uhalifu  hasa  katika maeneo yaliyombali na jeshi la polisi

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Katavi yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa