Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Na Walter
Mguluchuma
Katavi
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Wilaya
ya Mlele Mkoa wa Katavi kimejikuta kiko kwenye wakati mgumu baada ya kumwandikia barua ya
kumtambulisha kuchukua fomu za kugombea Pascal Mayala kwa msimamizi wa uchaguzi wa Jimbo la Kavuu kuwa ni mgombea Ubunge wa Jimbo la Kavuu
wakati kamati kuu ya Chama hicho
imemteuwa na kumtangaza mtu
mwingine kuwa ndio
mgombea wa Jimbo la Kavuu
Mayala ambae
alikuwa ni mshindi wa pili
kwenye kura za maoni za
chama hicho baada ya kushindwa na Laulent
Mangweshi alichukua fomu
hizo kwa msimamizi wa uchaguzi wa Jimbo la Kavuu katika ofisi ya
msimamizi wa uchaguzi wa Jimbo hilo
iliyoko Inyonga Wilaya ya Mlele
Mara baada ya
kukabidhi barua iliyokuwa ikimtambulisha
kuwa ni mgombea wa Jimbo hilo alianza mara moja kufuata taratibu za ujazazi
wa fomu hizo na kisha
alikwenda Mahakamani na kura
kiapo
Mgombea huyo alichukua fomu ikiwa ni
masaa machache kabla ya
kamati kuu ya chama hicho
kutangaza majina ya wagombea
Ubunge kupitia chama
hicho huku kamati kuu ya CHADEMA ikiwa
imemtangaza Laulent Mangweshi
kuwa ndio mgombea wao wa
CHADEMA wa Jimbo la Kavuu na sio
Pascal Mayala
Katibu wa CHADEMA
wa Mkoa wa Katavi Almasi
Ntije alieleza kuwa Viongozi wa
chama hicho wa ngazi ya Wilaya walifanya makosa
kumwandikia barua ya
kumtambulisha kwa msimamizi wa uchaguzi kuwa
Mayala ndio mgombea wa chama hicho
Alifafanua
kuwa kamati kuu ya Chama
hicho ndiyo yenye mamlaka
ya kuteuwa wagombea wa nafasi ya Ubunge
kwenye majimbo
Katibu huyo
alisema uongozi wa Chama
hicho unafanya utaratibu wa
kuwasiliana na mwanasheria wao ili waweze kumwandikia barua
msimamizi wa uchaguzi ili aweze kuondoa
jina la Pascal Mayala
kwenye nafasi ya kugombea Ubunge
wa Jimbo la Kavuu
Mwandishi wa habari hizi alipomtafuta Mayala
kwa njia ya simu yake ya mkononi
alieleza kuwa yeye yuko safari akiwa anatokea
mjini Mpanda kwenda Inyonga Wilayani
Mlele kwa lengo la kukabidhi fomu za kugombea Ubunge kwa msimamizi wa
uchaguzi wa Jimbo la Kavuu Mkoani Katavi
KATAVI YETU BLOG
KATAVI YETU BLOG

0 comments:
Post a Comment