Home » » MATOKEO ZA KURA ZA MAONI MKOA WA KATAVI KUPITIA CHAMA CHA MAPINDUZI -CCM

MATOKEO ZA KURA ZA MAONI MKOA WA KATAVI KUPITIA CHAMA CHA MAPINDUZI -CCM

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 

Na  Walter  Mguluchuma
Katavi
Mbunge aliyemaliza  muda wake wa jimbo la Mpanda  vijijini  Moshi Kakosa  ameshinda  katika   mchakato  wa kura za maoni  katika  Jimbo la  Mpanda  Vijini  za kuomba  ridhaa ya kuteuliwa kugombea Ubunge (CCM)
Kakoso  alishinda   baada ya kupata kura 7691  wagombea  wengin   walikuwa ni  Wiliamu Makufye   kura   2414, Abdalla  Sumry  Kura  2076,  God  Nkuba  1,696    Elizabath  Sultani  747 Chief   Charles  Malack 674 na   Rok  Mgeju  kura   134
Kwa  Jimbo  la  Mpanda  Mjini    Sebastiani  Kapufi  ameongoza kura za maoni kwa kupata  kura  7,190  Galus  Mgawe  amepata kura  2359 na   Gabriel  Mnyere   amepata  kura   2010
Jimbo  la  Kavuu   Pundensiana  Kikwembe   ameongoza kwa kupata  kura 5232  Mselemu   Abdalla  kura  587 na  Zumba  kura 4245
jimbo la  Nsimbo  Richald   Mbogo  ameongoza  baada ya kupata  kura  9367 akifuatiwwa   na  mfanyabiashara  maarufu wa Mkoa wa Katavi Hasasanal  Shabir  (DALA)8674
Jimbo la  Katavi  ameongoza    Eng   Izack  Kamwelwe ambae ni meneja wa Tanroods wa Mkoa wa  Katavi   aliyepata kura  4870 na kufutiwa na  Maganga  Kampala  aliyepata  kura  3926
Baada ya kutangazwa kwa matokeo hayo   baadhi ya wagombea wanafasi  hizo wametuma  malalamiko ya kupiga  matokeo  katika  majimbo  mbalimbali ya  Mkoa wa Katavi
Miongoni  mwa malalamiko  hayo wanayolalamikia ni kuwa   baadhi ya wagombea walioshinda kwenye kura  hizo wanadaiwa kuwa walishilikiana  na  baadhi ya viongozi wa chama   na nunua  kadi na kuwagawia   watu ili wawapigie kura  bila kujari itikadi za vyama vyao na umri wao
Pia katika  malalamiko yao wamedai kuwa  wagombea hao wametumia  magari yao kwa ajiri ya kubebea watu ili wakawapigie kura kwenye vituo na pia baadhi ya watu wamepiga kura zaidi ya moja kwenye vituo tofauti na  pia wamelelemikia kuwepo kwa vitendo vya Rushwa kwenye vituo vya kupigia kura
Wakati huo huo waliokuwa  wenyeviti wa  Halmashauri ya Nsimbo , Manispaa ya Mpanda  na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Mpanda wameshindwa kwenye mchakato wa kura za maoni
 Aliyekuwa Mwenyekiti wa Manispaa ya Mpanda  Enock  Gwambasa  ameshindwa kwenye  Kata ya Mpanda Hotel  Mohamed Assenga  aliyekuwa Mwenyekiti  ameshindwa  katika  kata   ya  Ugala  na aliyekuwa  mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Mpanda Yassin  Kibiriti ameshindwa katika  Kata ya Mishamo

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Katavi yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa