Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Na Walter
Mguluchuma
Katavi
jeshi la
Polisi Mkoa wa Katavi linamshikilia Raia wa Nchi ya Burundi aliyefahamika kwa jina la Michael Lubandaya (18) Mkazi wa Nyanza Nchini
Burundi huku akiwa anaishi
nchini bila kibali
Kamanda wa Polisi
wa Mkoa wa Katavi Dhahiri Kidavashari aliwaambia waandishi wa habari juzi kuwa
mtuhumiwa huyo alikamatwa hapo juzi majira ya
sita na nusu mchana huko katika
Kijiji cha Kibaoni Wilaya ya Mlele Mkoani
Katavi
Alisema kuwa mtuhumiwa alikamatwa
kufuatia taarifa za raia wema walizozitowa kwa jeshi la Polisi baada ya
kumtilia mashaka juu ya uraia wake
Kidavashari alieleza baada ya taarifa hizo
kulifikia jeshi la Polisi walifanya msako wa kumsaka mtuhumiwa huyo
na ndipo siku hiyo walipofanikiwa
kumkamata
Baada ya
kufanyiwa mahojiano ya kina na polisi mtuhumiwa
Michael Lubandaya aligundulika
kuwa amejihandikisha huko
Kakese Manspaa ya Mji wa
Mpanda katika daftari
la kudumu la wapiga kura
kwa jina la Abdallah Yusuph
Na alipatiwa
kitambulisho cha wapiga kura kilichotolewa na Tume ya uchaguzi ya Taifa chenye
namba t-1000-756-1
Kidavashari alisema
katika uchunguzi wa awali mtuhumiwa
alibainika kuwa sio rai wa Tanzania ni Raia wa Burundi na alijiandikisha kwenye daftari la kudumu la wapiga kura huku akitambua kufanya hivyo si
halali kufanya hivyo
Mtuhumiwa anatarajiwa kufikishwa mahakamani
mara baada ya uchunguzi utakapo kuwa
umekamilika ili ajibu mashitaka ambayo yanamkabili
0 comments:
Post a Comment