Home » » Wananchi epukaneni na wanao taka uongozi kwa njia ya Rushwa

Wananchi epukaneni na wanao taka uongozi kwa njia ya Rushwa

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 

Na  Walter  Mguluchuma
Katavi
Kiongozi wa  mbio za Mwenge wa Uhuru  Juma  Chum amewataka  Watanzania  kutowachagua viongozi wanao  taka   wachaguliwe kuongoza kwa kutumia Rushwa na  badala yake wawachague viongozi  bora  na waleta  maendeleo
Chum  alitowa  kauli  hiyo  hapo  juzi wakati   alipokuwa  akiwahutubia  mamia ya wanachi wa  Tarafa ya I Inyonga  Wilaya ya  Mlele  Mkoa wa Katavi  wakati wa  siku ya  mwisho ya mbio za mwenge uliokimbizwa  katika  Mkoa wa Katavi kwa muda wa siku nne
 Alisema wapo  baadhi ya viongozi  ambao wanataka kuchaguliwa  kuongoza  kwa njia ya kuwapatia wananchi Rushwa ili wawachague
 Alifafanua kuwa wapo  baadhi  ya  viongozi ambao wamekuwa wakitaka wachaguliwe kwa njia ya Rushwa na matokeo yake  baada ya kuchaguliwa wamekuwa wakishindwa kuwaletea wananchi maendeleo kwenye maeneo yao
Hivyo ni budi watanzania wakajitokeza kwa wingi kwenda kupiga kura za kuwachagua viongozi  kwenye uchaguzi mkuu wa Oktoba 25 na wawachague viongozi wale ambao watawaletea maendeleo
 Pia  aliwataka  wa wanafunzi wa shule za  Sekondari hapa  nchini wasome kwa bidii na kuachana na tabia ya kupata mimba za utotoni kwani hazina  manufaa kwenye maisha yao
 Alisema  wa  wapo baadhi ya wazazi wamekuwa na tabia ya  kuwazosha watoto wao  na kuwakatisha masomo  hivyo  wanafunzi hao  wajenge tabia ya kuwakatalia wazazi wao kuwakatisha masomo ili waolewe
Mbio za mwenge zimelaliza mbio zake za siku nne  katika  Mkoa wa Katavi  hapo  jana  ambapo  jumla ya miradi  yenye  thamani ya ziidi ya shilingi Bilioni  nne ilizinduliwa na kuwekwa jiwe la msingi katika Mkoa wa Katavi   na jana  Mwenge wa Uhuru ulikambiziwa  kwa  viongozi wa  Mkoa wa Tabora

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Katavi yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa