Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Na Walter
Mguluchuma
Katavi
Kiongozi wa mbio za
Mwenge Kitaifa Juma
Khatibu Chum ameipongeza
Halmashauri ya Manispaa ya Mpanda
kwa kutekeleza agizo la Rais kwa kujenga
vyumba vya maabara zilizokamilika
Chum alitowa
pongezi hizo hapo jana mara
baada ya kufungua majengo matatu
ya maabara ya shule ya Sekondari ya Kashaulili katika Manispaa ya Mpanda yaliojengwa na
kukamilika huku yakiwa na vifaa vya maabara vilivyokamilika na vimeanza kutumiwa na wanafunzi
Alisema
anaipongeza Manispaa ya Mpanda kwa kutekeleza agizo
la Rais kwani Halmashauri nyingi
ambazo mbio za Mwenge
zimepita wakekuta wamejenga majengo
tuu ambayo hayaja kamilika kwa kuwa hayana vifaa vya
maabara kama ilivyo Sekondari hiyo ya
Kata
Amlipongeza pia Mkurungezi wa
Manispaa hiyo Selemani Lukanga
kwa kuweza kusimamia na kufanikisha ujenzi wa maabara hizo
tatu za sayansi
Alisema
ukamilikaji wa maabara katika
shule za Sekondari utasaidia kupunguza tatizo la wataalamu wa fani
mbalimbali hapa Nchini kwetu
Chum alisema
kukamilika kwa maabara hizo tatu
leo hii tayari wanafunzi
wanao soma kwenye sekondari hiyo wameisha anza kunufaika
Alisema bila
kuwepo na maabara katika
nchi yetu hatuwezi kufikia
ulimwengu wa tatu tunaohitaji
kuufikia ili kuendana
na mabadiliko ya dunia
Mbio za mwenge
wa Uhuru jana zilianza mbio
zake katika Manispaa ya
Mpanda na miradi 14 ilipitiwa na
Mwenge wa Uhuru yenye thamani ya jumla ya Tsh1,364,224,845 nguvu ya wananchi ikiwa ni
Tsh70,710,791, Halmashauri Tsh 337,681,140 Serikali kuu
Tsh945,332,900 na wahisani walitowa
Tsh 10,500,000
0 comments:
Post a Comment