Home » » MIRADI YA ZAIDI YA SH BLIONI 4 KUTEMBELEWA NA MWENGE KATAVI

MIRADI YA ZAIDI YA SH BLIONI 4 KUTEMBELEWA NA MWENGE KATAVI

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 

Na  Walter  Mguluchuma
Katavi
 Jumla ya  miradi  ya  thamani ya  shilingi  bilioni  4,327,006,179  itatembelewa  na mbio za Mwenge  katika  Mkoa wa Katavi  ambapo  itazinduliwa  na  kuwekwa  jiwe  la  msingi  na  kukabidhiwa kwa walengwa
 Akizungumza  mara baada  ya kukabidhiwa  Mwenge  hapo  jana  na Mkuu wa  Mkoa wa Rukwa   Mwandisi Sitela  Manyanya  katika  Kijiji cha Sitalike  Wilaya ya Mlele   Mkoa wa Katavi  Mkuu wa  Mkoa  wa   Katavi  DR  Ibrahimu  Msengi alisema  miradi  itakayo  itakayozinduliwa  itakuwa 30
 Alifafanua  kuwa     Wilaya ya  Mpanda  itazinduliwa miradi  14na   Wilaya ya  Mlele  miradi 16  utawakeka  mawe ya msingi  miradi  nane  ambapo  wilaya ya  Mlele   utaweka  utaweka  mawe ya msingi  matano na  Wilaya ya Mpanda  mawe ya msingi matatu
 Katika  mbio  hizo   za  mwenge  ambazo  ujumbe  wa mwaka  huu ni  jiandikishe  kupiga kura  uchaguzi  wa mwaka 2015  baadhi ya miradi itawekwa  jiwe la  msingi  na  kuzinduliwa   Mkoani   Katavi
 Pia  utatowa  mikopo  na misaada  kwa vikundi  vya wanawake  watoto yatima  na  vijana  16  Wilaya ya  Mlele  na Wilaya ya Mpanda  vikundi  nane  ambapo  thamani ya miradi  yote  ni Tsh 4,327,006,179 ambapo  Tsh  587,404,021 ni  michango ya wananchi  Tsh 1,543,447,782 ni  Halmashauri  Tsh   1,516,584,,333 Serikali kuu na  Tsh  679,569,990 ni wahisani
Kwa  upande  wake  kiongozi  wa mbio za  mwenge  Kitaifa  Juma  Khatibu  Chum aliwataka  wananchi wajitokeze na kushiriki kwa wingi  katika uchaguzi mkuu wa mwaka huu
 Chum  alitowa wito kwa  wananchi  kuweza   kujitolea  katika  shughuli  za ukamilishaji  wa miradi ya maendeleo  katika maeneo yao
 Pia  aliwataka  watu waepukane na kutumia madawa ya kulevyo na  waepukane na watu wanaotaka uongozi kwa njia ya rushwa kwani Rushwa hurudisha nyuma maendeleo
Mwenge wa  ulianza mbio zake  hapo  jana   katika  Manispaa ya  Mji wa  Mpanda  na kesho utaanza  mbio zake  katika  Halmashauri ya Wilaya ya   Mpanda  katika  Mkoa wa  Katavi  utakimbizwa  jumla ya  kilometa  677.4 kwa muda wa siku nne  katika  Wilaya zote mbili za Mpanda na Mlele

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Katavi yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa