Home » » MBIO ZA UCHAGUZI 2015: WANA CCM 24 WARUDISHA FOMU ZA KUGOMBEA UBUNGE MAJIMBO YA KATAVI YUMO ARFI ALIYEKUWA CHADEMA

MBIO ZA UCHAGUZI 2015: WANA CCM 24 WARUDISHA FOMU ZA KUGOMBEA UBUNGE MAJIMBO YA KATAVI YUMO ARFI ALIYEKUWA CHADEMA

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 



Na  Walter  Mguluchuma
Katavi
Jumla ya wanachama 24 wa  CCM  katika  Mkoa wa Katavi wamerudisha fumu  za kuomba kuteuliwa kugombea   ubunge wa majimbo matano ya uchaguzi yalioko  Mkoa wa Katavi kupitia CCM
 Wagombea hao walirudisha fomu kwenye ofisi za   Wilaya  zao   hapo  juzi  ambapo  ndio ilikuwa siku ya mwisho ya watu kurudisha fomu za kuomba kugombea ubunge kwa ajiri ya kumpata mgombea  atakaye wakilisha  chama  hicho kwenye    uchaguzi  mkuu wa Oktoba 25 mwaka huu
Mkoa wa  Katavi unajumla ya  majimbo ya uchaguzi  matano   ambayo ni  Jimbo la  Mpanda  Mjini , Mpanda  Vjijini , Nsimbo , Kavuu na Jimbo la  Katavi
Waliorudisha  fomu kwa ajiri ya kugombea jimbo la  Nsimbo ni  Said  Amouri  Arfi ,Richald   Mbogo ,Hassanal   Shabir Dalla ,Manamba   David ,na  Frenk   Mapesa
Waliomba kugombea jimbo la  Kavuu ni watatu  ambao ni  Emanuel  Zumba ,Mselem Said  Abdalla  na   Mbunge wa viti maalumu  aliye  maliza  muda wake  Pudensiana Kikwembe
Jimbo la  Katavi lina wagombea  watano    Mwandisi  Izack   Kamwelwe, Maganga  Kampala ,Leph  Gembe , Shafi  Mpenda  na Osca   Albano  
Kwaupande wa  jimbo la Mpanda  Mjini   Katibu  msaidizi wa  CCM  Wilaya ya  Mpanda  Robart  Joseph  aliwataja waliorudisha fumu kuwa ni  Gabriel  Mnyere , Sebastiani  Kapufi  na  Galus  Mgawe  Jimbo la  Mpanda  Vijini    ni  Abdalla  Sumry , Moshi  Kakoso , Chifu     Charles  Malack ,Godfrey   Nkuba , Wiliam  Makufwe, Elizabeth   Sulutani   na  Rock  Mgeju
Kampeni za kujinadi wagombea hao  wa  zilianza  jana kwenye  majimbo ya  Mpanda  Mjini  na  Mpanda  vijini
 Kabla ya kuanza kwa  kampeni hizo za kujinadi kilifanyika kikao cha wagombea uchaguzi wa majimbo yote ambapo baadhi yao walitowa malalamiko ya kuanza kuchezeana  lafu kwa baadhi ya wagombea  wamekuwa wakitumia  kampeni za udini
Uchunguzi uliofanywa hivi  karibuni na mwandishi wa  habari hii hili umeweza kubaini kuwa kumekuwa na  tabia ya baadhi ya wagombea hao  kununua  kadi za CCM  kutoka  sehemu  nyingine  hasa  Dodoma na kuwaletea watu na kuwagawa bure  bila kujali  itikadi za vyama vyao ili  watu hao waweze kuwapingia kura  maonikwenye  mikutano mikuu ya Kata mbalimbali

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Katavi yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa