Home » » HII MBAYA SANA: MZEE WA MIAKA 70 AUWAWA KWA KUPIGWA NA WATU WASIOFAHAMIKA

HII MBAYA SANA: MZEE WA MIAKA 70 AUWAWA KWA KUPIGWA NA WATU WASIOFAHAMIKA


Na  Walter  Mguluchuma
Katavi
Mtu mmoja aliyejulikana kwa jina la  Paulo   Luzuba (70) Mkazi wa Kijiji cha Vikonge Wilaya ya Mpanda Mkoa wa Katavi  amefariki Dunia wakati akiwa anapatiwa matibabu katika Hospitali ya Wilaya ya Mpanda baada ya  kupigwa na watu wasiojulikana
Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Katavi Dhahiri Kidavashari marehemu huyo alifariki Dunia hapo juzi majira ya saa kumi jioni katika Hospitali ya Wilaya ya Mpanda  alikokuwa akipatiwa matibabu
Alisema kabla ya tukio hilo  siku ya  tarehe  16 machi  majira  ya saa nane  mchana  marehemu  aliondoka  nyumbani kwake kwa lengo la kwenda mnadani   kununua mahitaji ya  nyumbani kwake   akiwa na mjukuu wake  aliyejulikana  kwa jina  la  Wiliamu Shija(20)
 Alifafanua  walipofika kwenye eneo la mnada  marehemu alinunua mahitaji yake ya nyumbani chumvi,sabuni na dagaa na kisha  alimpatia mjukuu wake apeleke nyumbani na yeye alibaki kwenye eneo hilo la mnada
 Kidavashari alisema siku hiyo marehemu hakurejea tena  nyumbani  mpaka siku iliyofuata  ya tarehe 17 machi  majira ya saa nne  asubuhi  ambapo  marehemu alionekana karibu na eneo la mnadani  huku akiwa na majeraha usoni  na kichwani  na   huku akiwa uchi na akiwa amepoza fahamu
Marehemu alichukiliwa na ndugu zake  na  kupelekwa  Hospitali ya  Wilaya ya Mpanda  kwa ajiri ya maatibabu  ambapo  juzi alifariki  Dunia wakati akiwa anaendelea kupatiwa matibabu
Kamanda Kidavashari alieleza  mpaka sasa   chanzo cha  mauwaji  hayo bado   haijajulikana  na hakuna mtu wala watu waliokamatwa kuhusiana na  mauwaji hayo  na Jeshi la polisi kwa kushilikiana na uongozi wa Kijiji linafanya  upelelezi  ili kubaini  na kuwakamata  watu wote  waliohusika katika mauwaji ya Mzee huyo


    

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Katavi yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa