Na
Walter Mguluchuma
Katavi
Bodi ya maji ya
bonde la ziwa Rukwa imewahamasisha jamii ya watu
wanaoishi katika bonde godo la mto katuma
Wilayani Mpanda Mkoa wa Katavi nanma ya kusimamia na
kulinda rasilimali za maji
Viongozi wa Bodi
hiyo wamefanya uhamasishaji kwa kwa watu wa vijiji
nane ambavyo watu wake ni watumiaji wa maji ya bonde
la ndogo la mto Katuma wakati wa maadhimisho ya wiki ya maji
Akizungumza na
Wanachi wa Kata ya Mwamkulu hapo jana Afisa mahusiano
toka bodi ya maji ya bonde la ziwa Rukwa
Thadeus Ndeseiyo alisema bodi hiyo imekuwa ikifanya
shughuli za kusimamia uhifadhi wa mabonde madogo ya
mito iliyoko katika mikoa ya Katavi ,Rukwa Mbeya
Singida na Tabora chini ya ufadhili wa shirika la
GIZ la nchi ya Ujerumani
Alisema
lengo la bodi hiyo ni kuhamasisha jamii iliyopo katika
bonde la mto Katuma na maeneo mengine kusimamia
rasilimali za za maji ambazo siku hizi za karibuni zilikuwa
zimeharibiwa
Alisema
siku za hivi karibuni mto Katuma ambao ni tegemeo kubwa
la maji kwa wanyama wa hifadhi ya mbuga ya Katavi ambao
wanayatumia maji umekuwa na tabia ya kukauka mara kwa mara kutokana na
uharibifu wa mazingira
Nae Afisa
maendeleo wa bodi ya bonde la ziwa Rukwa Mgaujilwa
Watison alieleza kuwa uhamasishaji huu wa kuelisha jamii nanma ya
kutunza na kulinda Rasilimali za maji ni zoezi endelevu
Alisema
watu wanapaswa watambue kuwa swala la kulinda na kutunza rasilimali za
maji ni lalazima na sio jambo la hiari hivyo wananchi wanapaswa watambue hivyo
Mwenyekiti
wa umoja wa watumiaji wa Maji wa bonde la mto Katuma Gerald Majura
alieleza kuwa bado kuna changamoto ya watu bado hawajui
umuhimu wa vyanzo vya maji
Alifafanua
kuwa wapo baadhi ya watu bado wanafanyia shughuli za kibinadamu kwenye
vyanzo vya maji kwa kufugia mifugo yao
Kwa upande
mmoja wa wananchi wa Kijiji cha Mwamkulu Saimon Gwambi alisema kuwa
tangu kuanzishwa kwa jumuia ya watumiaji wa maji ya bonde dogo la mto
Katuma hapo mwaka jana faida zake zimeanza kuonekana
Alisema
Kwani uoto wa asili ambao ulikuwa umeisha potea umeanza
kuonekana baada ya watu kuelimishwa nanma ya kulinda
rasilimali za maji hivyo hari ya mazingira imeanza kurudi
kwenye hari yake ya kawaida
Kaimu
Katibu Tawala wa Mkoa wa Katavi Said Mwapongo alieleza kuwa
lengo la Serikali ni kuhakikisha kila mtu anapata huduma ya maji hivyo ni
vizuri rasimali za maji vitunzwe vizuri ili maji yasije
yakakauka
Katika wiki hiyo
ya maji viongozi wa bonde la ziwa Rukwa waliandaa mashindano ya
mpira wa miguu yaliyowashilikisha timu za vijana kwalengo la
kuwahamasisha vijana namna ya kuhifadhi mabonde
na vyanzo vya maji kupitia mashindano hayo ya mpira wa mguu wa
wanaume na wanawake kauli mbiu ya maji mwaka huu maji kwa
maendeleo endelevu
MWISHO
Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
0 comments:
Post a Comment